Na John Walter -Babati
Mashindano ya kumtafuta mrembo atakaetangaza madini adhimu ya Tanzanite kupitia jukwaa la Miss Tanzanite Manyara yanatarajiwa kufanyika usiku wa Novemba 16,2024 katika ukumbi wa kisora Hall Mjini Babati.
Mashindano hayo ambayo kwa mwaka huu yanawashiriki zaidi ya 12 kutoka mikoa mbalimbali nchini yametanguliwa na shindano la kusaka Top Model huku majaji watatu wakichuja na kuwatangaza warembo waliotisha kwa kuonesha vipaji vyao vya kuimba, ubunifu kwenye mavazi, kucheza na kuigiza katika hotel ya New Harambe mjini hapa.
Jaji mkuu Eva Godwin akisaidiana na Mbaraka Sungi na Lucy Kimaro wakiwatangaza Doreen Gasper mshiriki namba 5, Jennifer Mmary mshiriki namba 8 na Jackline Kagila mshiriki namba 7 kuwa washindi katika mavazi.
Washindi wengine ni wenye vipaji vya kucheza, kuimba na kuigiza ambao ni Amina Ramadhani mshiriki namba 11, Anelfaith Samwel mshiriki namba 6 na Rose Dickson mshiriki namba 2.
Akizungumza na Muungwana blog Mkurugenzi wa Kampuni ya Natha's Entertainment ambao ndiyo waandaji wa shindano hilo Aminatha Adolf Shamte, alisema tukio kubwa zaidi litafanyika Novemba 16 hivyo Wananchi wote wafike kwa wingi kushuhudia mrembo akivalishwa taji na burudani zingine zikitolewa.
Aminatha alieleza kuwa mshindi wa shindano hilo ataipeperusha bendera ya Manyara kote nchini na nje ya nchi katika kutangaza madini ya Tanzanite na vivutio vingine vilivyopo.
0 Comments