KAMPUNI ya Airtel imetangaza Washindi wa droo ya pili ya promosheni ya Santa Mizawadi inayotolewa na Bwana Santa kutoka Airtel.
Akizugumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Desemba 31, 2024 Meneja Mahusiano wa Airtel, Serikalini, Jennifer Mbuya amesema promesheni hiyo bado inaendelea na droo ya kwanza na pili zimetangazwa ambapo washindi ni kutoka mikoa mbalimbali nchini wamejishindia zawadi mbalimbali.
Washindi wa droo ya pili ni Ngusa Konzongwe kutoka Kariua mkoani Tabora amejishindia Simu Janja na mshindi wa pili wa simu janja ni Mangi Ibrahimu Kutoka Mwanza.
Na mshindi wa Luninga (Smart Tv) ni Saigule Mollel kutoka Wilaya Longido jijini Arusha na mshindi wa Milioni Moja ni Jumanne Kigomba kutoka wilaya ya Kibiti mkoani Pwani.
Washindi wengine ni Amani Kasisi, kutoka jijini Mbeya amejishindia Pikipiki mpya kabisa na Mshindi wa 5G routa, Batuli Shichambo kutokaTanga.
Jenipher amesema Airtel Santa Mizawadi ni promosheni kabambe ambayo itawapa washindi fursa ya kuondoka na zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim hadi shilingi milioni moja kila wiki kwa mwezi mmoja katika kipindi cha sikukuu.
"Jinsi ya kushiriki na kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, Wakala wa Airtel atatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha, ambapo pia ili Mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa tu kufanya miamala kama vile kununua bando, Kutuma pesa, kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa nje ya nchi, kununua muda wa maongezi.
Ndugu mteja , Wakala usipitwe na zawadi hizi kutoka kwa Mr Santa ambapo Jumanne Desemba 24 na 31 tumeshawatangaza washindi wa zawadi kutoka Airtel." Amesema Jenipher
Amesema droo ya kuwapata washindi wengine itakuwa ikifanyika jumanne mpaka mwezi wa kwanza ambapo washindi wakipigiwa simu kupitia namba 100 pekee na kuambiwa ni kitu gani ameshinda katika droo kama ilivyofanyika leo.
"Mteja wetu usikose kuendelea kutumia huduma zetu za Airtel ikiwemo kuweka Pesa na kutoa, kulipa bili mbalimbali ili kuweza kuingia katika droo ya kujishindia zawadi mbalimbali." Ameeleza Jenipher
Meneja Uhusiano kutoka Airtel, Jenipher Mbuya akizungumza jijini Dar Es Salaam leo Desemba 31, 2024, alipompigia mshindi wa Santa Mizawadi wa Airtel, zawadi hizo ni za kusheherekea sikukuu ya Christimas na Mwaka mpya pamoja na Airtel. Kulia ni Meneja Ubunifu kutoka Airtel, Husein Simba.
Meneja Uhusiano kutoka Airtel, Neema Mbuya akizungumza jijini Dar Es Salaam leo Desemba 31, 2024, wakati wa kutangaza washindi wa Santa Mizawadi wa Airtel, zawadi hizo ni za kusheherekea sikukuu ya Christimas na Mwaka mpya pamoja na Airtel.
0 Comments