F Askari polisi afariki kwa kugongwa na lori Babati | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Askari polisi afariki kwa kugongwa na lori Babati



Na John Walter -Babati

Askari kata wa kituo cha polisi Kiteto Geogre Mwakambonjo anaekediriwa kuwa na umri wa miaka 40 amefariki baada ya kugongwa na lori akiwa kwenye pikipiki mchana wa leo katika eneo la Msasani Maisaka wilayani Babati mkoani Manyara barabara ya Arusha dodoma. 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Manyara Ahmed Makarani amesema ajali hiyo imetokea leo Desemba 24,2024 baada lori iliyokuwa nyuma ya pikipiki hiyo kumgonga mwendesha pikipiki kwa nyuma na kusababisha kifo cha askari huyo aliyekuwa amebebwa na pikipiki hiyo. 

Kamanda Makarani amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori. Aidha, kamanda wa jeshi mkoani Manyara amesema hali ya ulinzi na usalama katika mkoa wa Manyara imeimarishwa na kuwataka wananchi kusherehekea siku kuu kwa amani na utulivu.

Post a Comment

0 Comments