MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Tanga Ramadhan Omari amewataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa walioshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27 mwaka huu kuwatumikia wananchi ili kutekeleza ilaniya Chama hicho kama ambavyo waliomba ridhaa ya kushika dola.
Hayo aliyasema wakati akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru wananchi kata ya Makorora iliyopo halmashauri ya jiji la Tanga kwa kuchagua wenyeviti na wajumbe kupitia Chama hicho ambapo katika alisema katika mitaa Sita ya kata hiyo wenyeviti wote na wajumbe wote wametokana cha hicho.i
Alisema kuw wananchi kata hiyo wameipa deni kubwa Chama hicho kwa kuendelea kukiamini Chama hivyo Chama kitaendelea kuwasikiliza wananchi kutatulia changamoto zilizopo kwenye mitaa yao kupitia wenyeviti wao .
Aliongeza kusema wameunga mkono Chama hivyo kwa kuwachagua viongozi wanaotokana CCM hivyo kitaendelea kuwaboreshea Miundo mindo bora katika mitaa yao ndani ya miaka mitano ya uongozi wao.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Omar Mzee alisisitiza kwamba kazi kubwa ya viongozi hao ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi wao kwa unavyotakiwa lakini pia watashirikiana kutoa mikopo ya asilimia kumi kwa vikundi walivyoomba wananchi wa Kat hiyo.
Aidha alisema yeye pamoja wevyeviti hao watashikiana pamoja kulitekeleza hilo ili kuweza kuwanufaisha wananchi wote bila kuwabagua kwa Imani zao wala vyama vyaox
sambamba na hayo aliwapongeza wananchi wote kata hiyo kuwachagua viongozi kupitia Chama cha mapinduzi CCM hivyo hawakufanya makosa badala yake watarajie kupata maendeleo..
0 Comments