Gekul amesema ni sehemu ya kupata faraja na kumrudishia Mungu shukrani kwa mapito magumu aliyopitia na kusema ni muda sasa wa wananchi kujua ukweli uliopo na kuacha kumnenea mabaya.
“Leo nimeshukuru kanisani na nadhani kuendelea kuhukumiwa kilasiku kwa masuala ya uongo si sahihi watu wajue ukweli, kwasababu kwa mwaka mzima huu wakati natuhumiwa watu wakiongea kama sio maombi yenu viongozi wa dini mimi binafsi nisingeweza kuishi tena.”
Aidha Gekul amesema ni dhahiri kuwa Mungu amemjibu maombi yake kwani hata ripoti ya kitabibu baada ya vipimo imeonesha wazi kuwa kijana huyo hakuwa na majeraha yeyote kwenye mwili wake wala dalili zozote za yeye kuingiziwa chupa sehemu ya haja kubwa na hata alivyofika kituo cha polisi alieleza kuwa amepigwa na mtu asiyejulikana, sasa ameamua kuyasema hayo ili watanzania wote wajue ukweli na kupunguza maumivu mazito aliyoyabeba tangu jambo hilo lilipozushwa.
“Walivyofika polisi, huyo kijana akasema amepigwa na mtu asiyejulikana, kwanini hawakwenda na kusema Paulina ndo amewapiga na kuwadhuru? Nimeona mwaka huu wakati namaliza nimshukuru Mungu moyo wangu niukung’ute niseme kila kitu ili na mimi nisiendelee kutembea kama roboti na kulia moyoni.”
Lakini pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutengeneza mazingira ya uwazi ya kufuatilia jambo hilo hadi pale lilipobainika kuwa ni batili baada ya mwendesha mashtaka wa serikali kutupilia mbali shauri hilo kwa kuwa lilikosa mashiko kisheria na kuishauri jamii endapo changamoto yoyote inatokea waliachie jeshi la polisi lishughulikie suala hilo ili lipate mwafaka mzuri na sio kuingilia kazi ya jeshi la polisi.
“Nimshukuru Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa alitoa nafasi nikapisha uchunguzi na ninaomba niwaeleze kuwa matatizo yanapotokea kwenye nchi yetu, yanapowapata wenzetu tuipe nafasi jeshi la polisi na vyombo vyake na serikali wachunguze, vinginevyo tumekuwa tukihukumu watu bila kuruhusu uchunguzi kufanyika.”
Kwa upande wao viongozi wa dini waliohudhuria hafla hiyo wamemsihi Gekul kuendelea kuchapa kazi kwani majaribu ni sehemu ya maisha ya mwanadamu na wameahidi kumuombea ili anedelee kuwatumikia wananchi wa jimbo la Babati mjini.
“mitihani na majaribu hayo ni mambo ya kawaida kwenye maisha, kitu ambacho napenda ukiweke moyoni ni kwamba umepita katika hayo yote si kama jiwe au ambao iliyoungua lakini ni kama chuma ili mbeleni ikatokee chuma bora zaidi.” Jasson Kahembe mchungaji wa KKKT Babati.
“Sisi tulioshiriki tumuombee mwenyezi Mungu ili mitihani inapokuja kama hivi awe ni mwenye kufaulu kwasababu Mungu akimpenda mja wake huwa anampa mitihani ili amwangalie atafaulu au atafeli, sasa mheshimiwa wetu Mbunge katika myihani huu amefaulu.”
Kwa Upande wake diwani wa Kata ya Kibosho kati Bahati Sebastian Mamboma, amewasihi wana Babati kufunga macho kwa hayo yanayoendelea kusemwa badala yake wajikite zaidi kuangalia maendeleo yaliyoletwa na Gekul ndani ya jimbo la Babati mjini tangu awe mbunge, kwani ni maendeleo makubwa sana hivyo wananchi waendelee kumpa sapoti ili aendelee luongoza zaidi na kuleta maendeleo makubwa kwa Babati.
“Wakati Chambiri anakabidhi hili jimbo kwa mheshimiwa Gekul Babati ilikuwa hivi ilivyo leo? Kwahiyo vita alivyonavyo sio vidogo na kila mmoja kwa nafasi yake na kwa namna yake anajaribu kuyafuta yale mazuri aliyoyafanya Gekul, niombe wanababati tushirikiana naye”
0 Comments