F itel Tanzania Yaunga Mkono Elimu Zanzibar Kupitia Mpango wa CSR | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

itel Tanzania Yaunga Mkono Elimu Zanzibar Kupitia Mpango wa CSR


ITEL, chapa ya kimataifa, imethibitisha tena kujitolea kwake kwa elimu na maendeleo ya jamii kupitia tukio la kurudisha  kwa Jamii (CSR) lililofanyika tarehe 4 Desemba 2024, katika Shule ya Msingi Kiwandui, Zanzibar. Mpango huu, kwa kushirikiana na Amity Foundation na Dream Public Welfare (DBSA), unalenga kusaidia shule za hapa kwa kutoa vifaa muhimu vya kujifunzia ili kuboresha fursa za elimu kwa wanafunzi wa jamii zenye uhitaji.

Tukio hili linaendana na maono makubwa ya itel ya kuunda mazingira ya kujifunza yenye usawa kote Tanzania. Itel ilitoa madawati, viti, na mbao za kuandikia Pamoja na vifaa mbalimbali kama mabegi ya shule na madafutari kwa shule za eneo hilo, kushughulikia changamoto kubwa za miundombinu ambazo mara nyingi zinakwamisha uzoefu wa wanafunzi kujifunza.

Akizungumza kwenye tukio hilo, Bruce Lu, Meneja wa Nchi wa itel Tanzania, alisisitiza umuhimu wa elimu kama msingi wa maendeleo endelevu. "Elimu ni msingi wa maendeleo, na kupitia mipango kama hii, itel imejipanga kuwawezesha vizazi vijavyo. Lengo letu ni kuhakikisha kila mtoto anapata rasilimali wanazohitaji ili kujifunza, kukua, na kufikia ndoto zao," alisema Bruce.

Mpango huu wa CSR unaendana na juhudi za muda mrefu za itel barani Afrika, ambapo chapa ya itel imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia elimu kupitia michango na miradi ya ushirikiano kwa zaidi ya miaka 10. Mpango huu wa Zanzibar unatarajiwa kuwa na athari za moja kwa moja kwa mamia ya wanafunzi, kwa kuwapa mazingira bora ya kujifunza na kuwahamasisha kufuata ndoto zao.

Tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi wa eneo, walimu, na wanajamii, ambao waliipongeza itel kwa kujitolea kwake kuboresha viwango vya elimu nchini Tanzania. Jitihada hizi za CSR pia ni hatua ya awali kwa mipango ya siku zijazo ya itel kupanua programu zake za “Love Always On,” zenye lengo la maendeleo endelevu na kuwawezesha jamii zenye uhitaji.









 

Post a Comment

0 Comments