Na John Walter -Babati
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda Desemba 12, 2024 ametembelea eneo lililoathirika na maporomoko kufuatia mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia Desemba 12, 2024 Tarafa ya Mbugwe, Kata ya Magara kijiji cha Moyamayoka.
Familia takribani 20 zimeathirika na maporomoko hayo huku upotevu wa mali na mifugo vikisombwa na maporomoko hayo.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ametoa pole kwa waathirika na kutoa rai kwa wananchi wa kijiji hicho kuacha tabia ya kukata miti kwaajili ya kuchoma mkaa kwenye maeneo ya mlimani ili kulinda maeneo hayo huku akizitaka kamati za maafa ya kata na ya Wilaya kuchukua hatua za haraka ili kuwasaidia waathirika ambao wamepoteza makzi yao.
0 Comments