F Mbunge Sillo apata alkasusi na wazee Galapo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mbunge Sillo apata alkasusi na wazee Galapo



Na John Walter -Babati

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ametembelea vijiwe vya Galapo jioni ya Desemba 30, 2024, na kushiriki kahawa na alkasusi pamoja na wazee na vijana wa eneo hilo.

Ziara hiyo ilikuja mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Galapo, ambacho kinajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 684 zilizotolewa na serikali.

 Ujenzi wa kituo hicho unalenga kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo, hususan kwa akina mama na watoto.

Akiwa kwenye vijiwe hivyo, Mbunge aliwasikiliza wananchi, akijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na kutoa ahadi ya kuzishughulikia kwa kushirikiana na serikali. Aidha, alitumia fursa hiyo kuhimiza mshikamano, ushirikiano, na juhudi za pamoja katika kuleta maendeleo ya jimbo hilo.

Wananchi wa Galapo walionesha furaha yao kwa hatua ya Mbunge kutenga muda wa kuzungumza nao katika mazingira yasiyo rasmi, wakisema kuwa kitendo hicho kinadhihirisha uongozi wa karibu na wananchi.

Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Galapo unatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2025, na wananchi wameelezea matumaini yao kuwa kituo hicho kitapunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za afya kwa jamii nzima.


Post a Comment

0 Comments