F Sillo awapongeza wazazi Babati kwa kutambua umuhimu wa Elimu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Sillo awapongeza wazazi Babati kwa kutambua umuhimu wa Elimu


Na John Walter -Babati 

Naibu Waziri Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo amewapongeza Wazazi wa wilaya ya Babati kwa kutambua umuhimu wa elimu katika kuikomboa jamii na kuhakikisha Watoto wao wanapata elimu bora. 

 Naibu Waziri ameeleza hayo wakati wa mahafali ya  wanafunzi wa awali katika shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza ya Sabnia sambamba na uzinduzi wa shule hiyo iliyopo Kata ya Galapo wilaya ya Babati mkoani Manyara Desemba 4, 2024

Mhe Sillo alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa sekta binafsi katika kuboresha elimu hivyo imejenga mazingira wezeshi na rahisi kwa wawekezaji katika sekta ya elimu. Alitoa wito kwa uongozi wa shule hiyo kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu na malezi bora ili taifa liweze kupata watu walioelimika na wenye taalumua mbalimbali 

Sambamba na hilo Mhe. Sillo amesema kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuendelea kuboresha mazingira mazuri ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati imejenga zaidi ya madarasa 180 Pamoja na kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo Kituo cha Polisi Galapo na kituo cha Afya cha kisasa kinachojengwa kata ya Galapo. Aidha aliwataka wananchi kuendelea kuunga mkono ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) kwa maendeleo ya wilaya hiyo

Post a Comment

0 Comments