F Waziri Jafo atoa maagizo kwa FCC kuhakikisha wanaimarisha mifumo ya kibiashara | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Waziri Jafo atoa maagizo kwa FCC kuhakikisha wanaimarisha mifumo ya kibiashara


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Selemani Jafo(Mb) ametoa rai kwa wawezekaji wazawa na wafanyabiashara kuhakikisha wanatumia fursa ya masoko mbalimbali ya ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora na kwa kuzingatia sera na taratibu za ushindani.

Ameyasema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani 2024 Desemba 5, 2024 Jijini Dar es Salaam ambapo maadhimisho hayo yameratibiwa na Tume ya Ushindani (FCC).

Waziri Jafo amesema fursa za masoko ya Ulaya, China na AGOA (Mpango wa Ukuaji na Fursa kwa Afrika unaowezesha mataifa ya Afrika kusafirisha bidhaa Marekani bila ushuru) zinaweza kutumika vyema kwa kuwa na kiwango kikubwa cha bidhaa zenye ubora mkubwa ambazo bila ushindani haziwezi kupatikana.

Aidha Dkt. Jafo ameuagiza uongozi wa Tume ya Ushindani (FCC) kuhakikisha wanaimarisha mifumo ya kibiashara nchini na michakato yote ya mapitio ya maunganiko ya kampuni wanayafanya kwa haraka lengo ni kusaidia vijana wa kitanzania wanapata ajira.

Vilevile Waziri Jafo amesisitiza juu ya umuhimu wa watumishi wa serikali kuchangia katika kuharakisha uwekezaji nchini ambapo aliwataka watumishi kutumia juhudi na maarifa yao kuhakikisha kila fursa ya uwekezaji inatimizwa kwa haraka na kwa ufanisi.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo ameagiza mijadala yote itakayojadiliwa katika maadhimisho hayo iwasilishwe kwake ndani ya siku kumi na nne ili kufanyia kazi mawazo yaliyojadiliwa kwa lengo la kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara na ushindani wa bidhaa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa FCC Dkt.Aggrey Mlimuka amesema kuwa tume hiyo inawajibu na kusimamia uwepo wa fursa sawa kwa washindani wakubwa na wadogo katika soko, na kupunguza ukiritimba katika masoko kwa kuhakikisha washindani wakubwa hawawazuii washindani wadogo kukua na kuingia au kuwatoa sokoni.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Wiliam Erio alisema hayo ni maadhimisho ya kwanza ya siku ya ushindani Duniani tangu kufanyika marekebisho ya sheria nchini.





 

Post a Comment

0 Comments