F Airtel yaendelea kumwaga zawadi kwa washindi wa promotioni ya ''Santa Mizawadi'' | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Airtel yaendelea kumwaga zawadi kwa washindi wa promotioni ya ''Santa Mizawadi''

DROO ya wiki ya tatu ya promosheni ya Santa Mizawadi inayoendeshwa na Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea ambapo wanawake wameng'ara zaidi.

Katika droo hiyo ya wiki ya tatu ambayo imechezeshwa leo, Januari 7, 2025  washindi wanne kati ya watano wamefanikiwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki ni wanawake.

Janeth Kwilasa, ambaye ni Meneja Mauzo kwa Wafanyabiashara wakubwa na Wadogo wa Airtel Tanzania, katika droo hiyo alimtangaza, Emanuela Vulwa kutoka Arusha kuwa mshindi wa Pikipiki.


Mshindi wa runinga smart, Inchi 55 alitangazwa kuwa ni Angelina Bahati mkazi wa Arusha.


Pia mshindi Shilingi wa mil 1 ni Elizabeth Robert kutoka Singida na mshindi wa Simu Janja alitangazwa kuwa ni Subira Omari wa jijini Tanga.


Katika droo hiyo mshindi pekee mwanaume ni Habibu Abdul wa Kagera ambaye ni mfanyabiashara aliyejishindia simu Janja.


Baada ya droo hiyo kuchezeshwa Maneja Mauzo wa kampuni hiyo, Kwilasa, amesema promosheni hiyo inaendeshwa kwa uwazi chini ya Bodi ya Usimamizi ya Michezo ya Kubahatisha.


Akielezea namna ya kushiriki na kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, Mmbando amesema Kwa Wakala wa Airtel anatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha na Kwa mteja anachotakiwa kufanya kununua bando, kulipa bili, kutuma na kutoa fedha, kununua muda wa maongezia au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60# au kupitia 'My Airtel App'.


 Ameongeza kuwa washindi wote watafikishiwa zawadi popote walipo baada ya taratibu kukamilika.


Pia ameongeza kuwa promosheni hiyo inafanyika ili kurudisha shukrani kwa wateja wao  wanaotumia mtandao wa Airtel kufanya miamala mbalimbali na kuendeleza shangwe.

Post a Comment

0 Comments