F CCM Manyara wamlilia Ester Mahawe | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

CCM Manyara wamlilia Ester Mahawe



Na John Walter -Manyara
Habari za kusikitisha zimepatikana leo, Januari 14, 2025, kuhusu kifo cha Ester Alexander Mahawe, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi iliyopo mkoani Songwe. 

Ester amefariki dunia katika Hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mheshimiwa Peter Toima, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara, ameomboleza kifo chake akimtaja kama mtu mwema na mwenye ushirikiano wa karibu na chama. 

Ester alikuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kupitia Jimbo la Babati Mjini na aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara kati ya mwaka 2015 hadi 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, akieleza masikitiko yake na kutoa pole kwa familia, ndugu, na watanzania wote walioguswa na msiba huu.

Marehemu Ester Alexander Mahawe atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya jamii na uongozi wake wa mfano. 

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.

Post a Comment

0 Comments