F Dkt.Scholastika ataka UWT kufanya siasa za kuisaidia jamii,afika Makete kumuona mhitaji | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Dkt.Scholastika ataka UWT kufanya siasa za kuisaidia jamii,afika Makete kumuona mhitaji

 





Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Dkt.Skolastika Kevela ameitaka jamii kuendelea kusaidia watu wenye uhitaji kupunguza changamoto wanazokumbana nazo hali inayoweza kuwarejeshea tabasamu na kujiona watu wa muhimu katika jamii.  

Dkt.Skolastika Kevela ametoa kauli hiyo wakati akitoa msaada kwa familia ya Nicko Mbwilo mkazi wa mamlaka ya mji mdogo wa Iwawa ambaye mtoto wake wa umri wa miaka 21 Amos Mbwilo amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa TB na Uti wa mgongo kwa muda mrefu sasa.

"Mtoto kama huyu tukimpa thawabu yetu inaandikwa mbinguni na tukumbuke mwenyezi Mungu akikupa basi kata kidogo na upeleke kwa wahitaji"amesema Dkt.Kevela

Rehema Pella ambaye ni mama wa mtoto na Niko Mbwillo baba wa familia wamesema mtoto huyo hajiwezi kwa huduma za msingi hivyo kulazimika kumhudumia Kwa Kila kitu ikiwemo kumpeleka maliwatoni.

"Pia amepata vidonda mpaka mgongoni sasa uwezo wa kukaa na kulala sana hana tunabaki tunamgeuza usiku na mchana ninapoenda kwenye kazi za mikono mwenzangu anabaki na kijana lakini pia alizaliwa na jicho dogo ila TB ndio iliyomsumbua"amesema Rehema Pella

Baada ya kuona Hali ya familia hiyo Hawa Kada makamu mweyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete amesema wao kama madiwani wataenda kuhakikisha mtoto huyo anapata bima kubwa itakayo wezesha kupata matibabu kila yanapohitajika ili kuwapunguzia gharama za matibabu wazazi.

Post a Comment

0 Comments