Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amtaka mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kutogombea tena nafasi hiyo kama alivyoshauriwa na familia yake.
Lema ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema mara kadhaa Mbowe amekuwa na nia ya kupumzika na kuwaachia nafasi vijana lakini wanachama wamekuwa wakimshauri kuendelea kuwa katika nafasi hiyo.
Amesema anamuheshimu sana Mbowe kwa kazi kubwa aliyoifanya hasa ya kukijenga chama hicho lakini anamuomba kwa sasa asikilize ushauri wa familia yake inayomtaka kutogombea nafasi hiyo.
0 Comments