Na John Walter -Babati
Maaskofu mbalimbali wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) leo Januari 15, 2025, wamehudhuria ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mchungaji wa kanisa hilo, Zebedayo Diiwasl Mahawe, aliyezikwa katika makaburi maalum ya Kanisa la Usharika wa Babati Mjini.
Mchungaji Mahawe, aliyezaliwa mwaka 1945, aliishi maisha ya utumishi wa Mungu kwa miaka mingi, akihudumu katika majimbo mbalimbali ya KKKT. Alifariki dunia Januari 10, 2025, na ameacha alama kubwa katika maisha ya kiroho na kijamii.
Ibada ya mazishi imeongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dk. Godson Abel Mollel, ambaye amewataka watoto kuwatunza wazazi wao kama ishara ya heshima na upendo.
Katika hotuba yake, Askofu Mollel amemsifu Mchungaji Mahawe kwa utumishi wake mwaminifu na mchango wake mkubwa katika kueneza injili na kuwahudumia waumini.
Mazishi hayo yamehudhuriwa na waumini, viongozi wa dini, familia, na marafiki wa marehemu, wote wakimkumbuka kama kiongozi aliyekuwa na moyo wa kujitoa kwa ajili ya kanisa na jamii.
Mchungaji Mahawe ameacha urithi wa kipekee wa imani na utumishi, akiwa mfano wa kuigwa kwa viongozi wa dini na waumini wa KKKT.
0 Comments