F Mati na NMB zatishana nguvu mechi ya kirafiki | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mati na NMB zatishana nguvu mechi ya kirafiki


Na John Walter -Babati
Kampuni ya Mati Super Brands Ltd imekutana na Benki ya NMB katika mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu iliyochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Singe, Mjini Babati.

Mkurugenzi wa Mati Super Brands Ltd, Bw. David Mulokozi, ambaye pia alishiriki katika mchezo huo, amesema lengo kuu la mechi hiyo ni kudumisha mahusiano mazuri kati ya kampuni yao na Benki ya NMB pamoja na kuhimiza mazoezi kwa ajili ya kuboresha afya.

Bw. Mulokozi ameongeza kuwa ushirikiano wa karibu na wafanyakazi wake kupitia shughuli mbalimbali kama michezo umekuwa chachu ya kuongeza ufanisi kazini, kwani huwahamasisha wafanyakazi kujituma zaidi.

Kwa upande wake, Donald Kipunga, Mdhibiti Ubora wa Tawi la NMB Babati, amesema wamefurahia sana mchezo huo na wanalenga kupanga mechi nyingine ya marudiano siku za usoni.

Mchezo huo uliokuwa wa ushindani mkubwa ulimalizika kwa timu zote kutoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1.

Post a Comment

0 Comments