Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Njombe Dkt.Scholastika Kevela ameagiza uongozi wa Jumuiya hiyo ngazi za wilaya kuhakikisha unajenga nyumba za viongozi ili kwenda sambamba na malengo ya Jumuiya.
Dkt.Scholastika ametoa maelekezo hayo kwa viongozi aliposhiriki baraza la UWT wilaya ya Ludewa.
"Ilitakiwa mje juu (kwenye vikao ngazi ya taifa) mkaone moto tunaoota kule juu ni mgumu sana,sasa kama huna kiwanja mwenyekiti wawilaya hakikisha umenunua kama una kiwanja basi pandisha nyumba na kama ipo kwenye renta uwe umepaua kwa maana UWT taifa watakuja kukagua hizi nyumba wilaya kwa wilaya"amesema Dkt.Sholastika
Aidha Dkt.Scholastika amechangia mifuko 10 ya saruji ili iweze kusaidia ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Jumuiya hiyo wilaya ya Ludewa.
Vile vile ameendelea kurudisha tabasamu kwa watu wenye uhitaji mkoani humo ambapo akiwa wilayani Ludewa amemkabidhi kiti mwendo Augenia Mtweve (27) ikiwa ni mwendelezo wake katika kuisaidia jamii.
0 Comments