KAMPUNI ya Oryx Gas imesema katika mwaka 2025 imeweka mikakati mbalimbali ya kufanikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutoa mitungi ya gesi na majiko yake kwa makundi mbalimbali.
Aidha imesema tangu mwaka 2021 mpaka mwaka 2024 imegawa bure mitungi ya gesi na
majiko yake zaidi ya 87000 na kwamba wataendelea na mkakati wa kuendelea kunamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia Mawakala wake walioko nchi nzima.
Akizungumza wakati wa kikao kazi cha mwaka 2024 kampuni hiyo ambapo kimewakutanisha mawwala wake kutoka mikoa yote nchini ,Meneja Mauzo na Msimamizi wa Masoko Oryx Gas Tanzania Shaban Fundi amesema wanajivunia kuwa sehemu ya kufanikisha matumizi ya nishati safi nchini.
Oryx Gas tumefika katika mikoa mingi sana tukihamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na mwaka 2024 peke yake tumetoa mitungi ya gesi isiyopungua 39,000 kwa mpango Maalum wa kusaidia Kaya mbalimbali pamoja na mbalimbali ya kijamii kwa kuwapatia mitungi ya gesi na majiko yake.
“Na wao wananchi wamekuwa mabalozi wa kuhahamasisha nishati safi ya kupikia na ukiangalia sio mwaka 2024 peke yake tumeanza tangu mwaka 2021 na ukiangalia tumetoa mitungi inayofikia 87000 mpaka sasa tena bure kabisa kwa ajili ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia
“Na hii ni kwasababu tunaunga mkono juhudi za Serikali ambayo nayo imeendelea kuhamasisha matumizi ya nishati na ndio kupitia Wakala wa Umeme Vijijini(REA) tumeona wanahamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia,”amesema Fundi.
Ameongeza kuwa wao kama Oryx wataendelea kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia na hiyo inawezekana kupitia Mawakala kutoka nchi nzima ambao wamekutana mwanzo
wa mwaka 2025 kwa ajili ya kuweka mikakati ya kwenda kutekeleza nishati safi ya kupikia nchini
Muhusu mkutano wa mawakala wa Oryx Gas,Fundi amesema ni mkutano wao mkuu mwaka ambapo kampuni inaangalia utendaji wake wa mwaka 2024 na kupanga mikakati kwa mwaka 2025.
“Kwahiyo huu ni mkutano ambao unajumuisha mawakala wote nchi nzima ambao wako katika maeneo mbalimbali na sisi Oryx tunajivunia kuona tuna mawakala kila mkoa,kila wilaya pamoja na vijijini na ndio maana tunajidhatiti na kujipambanua kwamba tunauwezo wa kufikisha nishati safi ya kupikia katika maeneo yote nchini Tanzania ikiwemo na Zanzibar.
“Mkutano huu ni mkubwa na unatoa dira ya kampuni kuelekea mwaka 2025,kwahiyo pamoja na hayo tunatoa mwito kwamba wananchi waendelee kupokea matumizi ya nishati safi ya kupikia na Oryx tumejipanga kısawasawa kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa kila Mtanzania.”
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Oryx Zanzibar Shuwekha Omar Khamis amesema kukutana kwa mawakala hao kuna maana kubwa katika kuthibitisha dhamira ya kampuni hiyo kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi na kila mwaka wamekuwa wakikutana na kuangalia walikotoka na kuweka mipango mipya kufikia malengo yao.
Kuhusu matumizi ya nishati safi Zanzibar amesema kwa sasa yameongezeka kwani mwaka 2020 yalikuwa asilimia 7.7 ya usambazaji wa nishati safi na mwaka 2024 yamefikia asilimia 26.5 na hiyo inamaanisha toka mwaka 2020 matumizi yao Zanzibar yametoka tani 3600 mwaka hadi kufikia tan 12400 mwaka 2024.
“Hii inakupa picha kuwa Wakazi wa Zanzibar wamebadilika,wameamka kutoka katika kutumia nishati chafu na kuingia katika nishati safi.Oryx Gas tumefanya jitihada kubwa katika kuwabadilisha wananchi wa Zanzibar kutoka katika nishati chafu kwenda kwenye nishati safi kwani tumechangia mitungi ya bure ambayo ni 18000 kwa mwaka 2024
“Nawaomba wananchi wa Zanzibar waondokane na matumizi ya kuni na mkaa ambayo sio salama kwa afya yetu na mazingira.Wengi wetu tunapata madhara yanayotokana na matumizi ya kuni na mkaa na tunatumia gharama kubwa kujitibu.”Amesema
Shuwekha Omar Khamis.
0 Comments