Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro limetoa angalizo kwa wamiliki wa kumbi za Starehe na sehemu za Starehe ikiwemo Baa kuhakikisha wanafuata Masharti ya Leseni Zao zinavyoelekeza muda halisi wa kufunga na kuepuka kujaza watu kuzidi uwezo wa eneo husika.
Akizungumza jana jumamnne Didemba 31 2024 Kamanda wa polisi Mkoani Kilimanjaro Simon Maingwa amesema jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha ulinzi na Usalama kwa raia hivyo ni wajibu wa wananchi nao kuchukua tahadhari wanapokuwa maeneo mbalimbali ikiwemo sehemu za starehe.
wamiliki wa baa na kumbi za starehe wazingatie masharti ya leseni zao ambayo inaonyesha muda halisi wa kufunga na kuepuka kujaza watu kupita uwezo stahiki wa maeneo yao ya biashara
Kwa upande wa upigaji wa fataki watakaoruhusiwa ni wale tu ambao watakao kuwa na vibali na hawataruhusiwa kufyatua katika makazi ya watu,vituo vya Afya na wazingatie masharti ya vibali hivyo.
Aidha Kamanda Maingwa ametoa onyo kwa watoto kutoruhusiwa kwenda kwenye Mikesha wa Sikukuu kwa Usalama wao,huku akiwaomba wazazi na walezi kuzingatia usalama wa nyumbazao kutoziacha bila uangalizi wanapokwenda katika Mkeshawa sikukuu ya Mwaka Mpya 2025.
Kamanda Maingwa amewasihi madereva na watumiaji wa vyombo vya Usafiri kutotumia vileo na kuendesha vyombo hivyo ili kuepusha ajali za barabarani ambapo Leseni za udereva 64 zimefungiwa kwa kipindi cha januari hadi Disemba 2024.
Makosa haliyopelekea kufungiwa Leseni hizo ni Mwendokazi Leseni 22,ajali 32,Ulevi 3,na kuyapita magari mengine bila tahadhari ni leseni 7.
0 Comments