F RC Simiyu aanza kwa kishindo ziara ya kijiji kwa kijiji ''tupo hapa kutekeleza maagizo ya Rais'' | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

RC Simiyu aanza kwa kishindo ziara ya kijiji kwa kijiji ''tupo hapa kutekeleza maagizo ya Rais''


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ametuagiza viongozi wote kwenda kuwatumikia wananchi katika maeneo ambayo tumekabidhiwa dhamana hii.

Sasa mimi niko tayari kuanzia leo kuja katika vijiji vyenu kusikiliza changamoto zinazowakabili maana kupitia nyie Wananzengo ndipo tunapoibua matatizo mbalimbali, kero zinazowakabili huku ikisaidia pia kujua wapi pana shida ikiwemo ukosefu wa huduma muhimu kama umeme, maji, afya, elimu, ukosefu wa pembejeo na hata miundombinu korofi ya barabara.

Maendeleo ya watu katika mikoa, wilaya, Vijiji na hata vitongoji, kwa kuliona hilo ndio maana nimeanza ziara ya siku 30 kwenda kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi katika vijiji vyote vya mkoa wa Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi ameyasema hayo wakati akianza ziara hiyo katika  vijiji vya Nyamikoma, Mwandama, Sapiwi, Igegu Magharibi,Igegu Mashariki, Igegu, Isenge, Mwamabu, Igagalulwa, Sengerema na Majengo.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Post a Comment

0 Comments