Takiribani Wakimbizi 5000 kati ya 135,000 waliopo katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wamenufaika na Misaada ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 100 kutoka Kampuni ya Itel Tanzania kwa kushirikiana na shirika la wakimbizi duniani UNHCR.
Misaada hiyo imetolewa na Meneja Masoko kutoka kampuni ya Itel Tanzania Bi. Sophia Almeida Mafiri na kukabidhi kwa mkuu wa kambi hiyo Ndg. Siasa Manjenje, na kusema wamekabidhi misaada ya vitu hivyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.
“Sisi kama Itel Tanzania tumeungana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Duniani (UNHCR) kwa ajili ya kuleta Misaada kwa wakimbizi hapa Nyarugusu na misaada ambayo tumeitoa leo ni Pisi 5000 ya vyandarua, Vitenge, Kanga, taulo za kike na nguo za ndani za watoto, wanawake na wanaume vyenye Thamani ya zaidi ya million 100” Amesema Bi, Sophia Almeida.
Kwa Upande wake Mkuu wa shirika la wakimbizi (UNHCR) Wilaya Kasulu Bw. Jean Bosco amewashukuru Itel kwa misaada ya waliyoitowa na kuwaomba waenendelea kutoa misaada kila wanapopata nafasi huku akibainisha shirika la (UNHCR) linapitia changamoto za kifedha ambapo imekuwa ngumu kuisaidia serikali kutatua changamoto kwa wakimbizi.
“Kwanza niwashukuru Itel kwa kutupa sapoti ambayo wameitoa kwetu na ni kweli taasisi yetu inapitia changamoto za kifedha hivyo imetufanya tushindwe kuisaidia serikali ya Tanzania katika kuwasaidia wakimbizi waliopo Tanzanzania hivyo kilio cha wakimbizi sasa kimesikika na Itel wameweza kusaidia hivyo Itel asanteni sana na karibuni tena” Amesema Bw. Jean.
Katika hatua nyingine mkuu wa Kambi Ndg. Siasa Manjenje amesema misaada hiyo itasaidia wakimbizi waliopo katika kambi hiyo kulingana na Idadi ya vitu walivyopokea kutoka Itel Tanzania huku akitoa wito kwa mashirika mengine kujitokeza kusaidia wakimbizi waliopo Nyarugusu.
“Tunawashukuru Itel kwa misaada waliyoitowa kwani itaenda kusaidia watu wengi maana katika kambi kuna watu wengi wenye uhitaji hivyo natowa wito kwa mashirika mengine ya kiserikali na mashirika ya watu binafis pamoja na watu wengine tunawakaribisha sana Nyarugusu”Amesema Manjenje.
0 Comments