F Wassira apendekezwa kurithi kiti cha Kinana | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wassira apendekezwa kurithi kiti cha Kinana



Na John Walter

Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa imewasilisha jina la mwanasiasa mkongwe nchini 
Stephen Wasira kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa CCM Taifa unaofanyika Jijini Dodoma, kwa ajili ya kupigiwa kura kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara. 

Wasira aliyezaliwa Julai Mosi, 1945 wilayani Bunda Mkoa wa Mara, kwa zaidi ya nusu karne amejijengea heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika siasa, uchumi na maendeleo ya jamii.

Wasira ni miongoni mwa wana CCM waliowahi kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Ni mmoja wa viongozi wakongwe wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM, ambapo tangu mwaka 2007 amekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tangu mwaka 2011.

Amekuwa mbunge wa Jimbo la Bunda mkoani Mara na waziri wa wizara mbalimbali nchini katika awamu tofauti tofauti.

Rekodi yake ya uongozi na uchapakazi wake, imemuweka kuwa katika nafasi nzuri ya kuonekana kama nguzo muhimu ndani ya CCM.

Post a Comment

0 Comments