Serikali imezishauri taasisi mbalimbali nchini kujiorodhesha kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki kukuza uchumi wao binafsi na uchumi wa nchi kwa njia za kidijitali.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), wakati wa hafla ya kuorodhoreshwa rasmi kwa Hati Fungani ya Benki ya Azania ijulikanayo kama Bondi Yangu, katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, hafla iliyofanyika katika Ofisi za DSE, jijini Dar es Sal
Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa Uorodheshwaji wa Hatifungani hiyo utakuza ukwasi kwa wawekezaji kwa kutoa mwanya wa kuuza na kununua kupitia soko hilo na utaleta chachu kubwa katika kukuza Soko la Hisa la Dar es Salaam ambalo limekuwa mstari wa mbele katika kutoa fursa kwa watanzania kushiriki katika sekta rasmi ya fedha.
“Taarifa mbalimbali zilizotolewa zinaonesha mauzo ya Bondi Yangu yamekuwa ya mafanikio makubwa kwa kukusanya jumla ya Shilingi bilioni 63.3 ambayo ni mafanikio ya asilimia 210.9, mafanikio ya namna hii ni nadra kwa mtoaji wa kwanza wa Hatifungani na hii inadhihirisha kuwa Benki ya Azania imeanza na mwanzo mzuri wa utoaji wa Hatifungani yake na malengo yao ni kukusanya zaidi ya TZS 100 bilioni ili kusaidia makundi ya wanawake, vijana na wajasiriamali wadogo kuweza kushirikishwa katika sekta rasmi ya fedha hapa nchini” alisema Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA), CPA. Nicodemus Mkama amesema kuwa mauzo ya hatifungani ya benki ya Azania yamepata mafanikio ya asilimia 210.9, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 63.27 kimepatikana ikilinganishwa na shilingi bilioni 30 zilizopangwa kupatikana.
“Mafanikio
haya yana maana kubwa katika ustawi na maendeleo ya sekta ya fedha,
kwani inaonesha imani waliyonayo wawekezaji kwa benki ya Azania na
masoko ya mitaji, ambapo masoko ya mitaji hapa nchini yamekuwa na bidhaa
mpya na bunifu zinazokidhi matakwa ya wawekezaji wa ndani na wa
kimataifa,”amesema CPA.Mkam
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Dkt Esther Mang’enya amesema mauzo ya hatifungani hiyo imevuka lengo la asilimia miambili na kumi.
Peter Nalitolela ni Afisa Mtendaji Mkuu soko la Hisa la Dar es salaam –DSE amesema uwekezaji katika soko hilo imeendelea kuongezeka ambapo hadi kufikia januari 23 mwaka huu zaidi ya laki 6.
Hatifungani ya Benki ya Azania benki ilianza mwezi Novemba na kufungwa mwezi Disemba mwaka jana pamoja na kupewa idhini kutoka mamlaka ya masoko ya mitaji kuongeza kiwango ya kuchukua zaidi ya fedha iliyopatikana.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akigonga kengele kuashiria kuorodhoreshwa rasmi kwa Hati Fungani ya Benki ya Azania ijulikanayo kama Bondi Yangu, katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Hafla iliyofanyika katika Ofisi za DSE, jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine aliziasa taasisi zingine kuiga mfano wa Azania Bank wa kujiorodhesha kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam na kutoa fursa kwa wananchi kushiriki kukuza uchumi wao binafsi na uchumi wa nchi kwa njia za kidijitali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Esther Mang'enya akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa toleo la kwanza la hatifungani ya Benki ya Azania (Azania Bond Yangu) katika Soko la Hisa la Dar es Saaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA), CPA. Nicodemus Mkama wa pili kutoka kushoto akimuonesha jambo Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa toleo la kwanza la hatifungani ya Benki ya Azania (Azania Bond Yangu) katika Soko la Hisa la Dar es Saaam leo.
0 Comments