F Airtel Tanzania na Tuzo za Trace Washirikiana Kuinua Muziki wa Kiafrika | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Airtel Tanzania na Tuzo za Trace Washirikiana Kuinua Muziki wa Kiafrika

Dar es Salaam, Airtel Tanzania imetangaza ushirikiano wake na tuzo na mkutano wa Trace kwa mwaka 2025, ambao unatarajiwa kufanyika Mora Resort visiwani Zanzibar kutoka Februari 24 hadi 26. Ushirikiano huu ulitangazwa kabla ya tukio hilo la siku tatu ambao utasheherekea mzuiki wa Kiafrik, uvumbuzi na utamaduni unaowaleta Pamoja vinara wa muziki wa Afrika.  

Akizungumza wakati wa hafla maalum ya kutangaza ushirikiano huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Timea Chogo, alisisitiza juu ya umuhimu wa kuunganisha teknolojia na burudani kutengeneza fursa mpya kwa ajili ya wasanii wadogo na watumiaji wa kidijitali nchini Tanzania.

“Tuzo na Mkutano wa Trace ni jukwaa linalotambulika duniani ambalo linasheherekea vipaji bunifu Pamoja na kuchochea ukuaji wa kidijitali barani Afrika. Ushirikiano unaenda sambamba na kampeni ya SmartaWithData ya Airtel Tanzania ambayo inawawezesha kufanya maamuzi mazuri, kusimamia vizuri matumizi yao na kufurahia huduma za mtandaoni kwa thamani na umiliki mkubwa,” alisema Chogo.

Pia aliongeza kuwa ushirikiano huu unahakisi maono ya pamoja ya Airtel Tanzania na Trace katika kuwapatia vijana vifaa na majukwaa ambayo wanahitaji kujieleza, kuunganishwa na fursa kuweza kupata mafanikio katika zama hizi za kidijitali.

Kama sehemu ya ushirikiano huu, Tanzania itakuwa mwenyeji wa Trace Tour kutokana na mafanikio yalipatikana nchini Kenya na katika maeneo mengine ambayo ni masoko ya Airtel. Mpango huu unalenga kuleta uzoefu wa kipekee kwa mashabiki Pamoja na wasanii hali itakayoimarisha nia ya Airtel ya kuitajirisha sekta ya burudani na sekta ya kidijitali.

“Data ni lango muhimu la muziki, elimu, biashara na burudani. Kupitia SmartaWithData tumejidhatiti kuwasaidia watumiaji kutumia kikamilifu data huku wakiendelea kuunganishwa na mtandao kwa wepesi,” aliongeza Chogo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Trace East Africa, Danny Mucira, alieleza namna muziki ulivyo na nguvu ya kuunganisha tamaduni mbalimbali huku akibainisha mchango wa muda mrefu wa Trace katika kuutangaza muziki, vipaji na tamaduni za kiafrika.

“Mziki ni lugha inayozungumza na kila mtu duniani, na pia kwa kushirikiana na Airtel tunatengeneza fursa hii kwa ajili ya wanamuziki chipukizi kwa kuwapatia nyenzo za kidijitali na namna ya kuwafikia mashabiki zao ili waweze kufanikiwa katika dunia ya sasa,” alisema Mucira.

Akiongeza katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti, Dk. Obi Anyalebechi, alisisitiza jinsi hafla hiyo inakavyoboresha sekta ya utalii nchini, akibainisha kuwa itavutia watazamaji wa kimataifa na kuiweka nchi kama kivutio bora cha utalii duniani.

"Utalii ni nguzo muhimu ya uchumi wa Tanzania, na lengo ni kuongeza wageni wa kila mwaka kutoka milioni 3 hadi milioni 10 ifikapo mwaka 2030. Kuandaa hafla ya kiwango hiki sio tu kutavutia wageni wa kimataifa bali pia kutaongeza mwonekano wa Tanzania duniani kote, kuhimiza wasafiri zaidi kutalii nchi na kuchangia katika ukuaji wa sekta ya utalii," alisema.

Tuzo za Trace na Mkutano wa 2025, unaoendeshwa na Airtel Tanzania, unatarajiwa kuwa tukio la kihistoria la kusherehekea makutano ya muziki, utamaduni, na ubunifu wa kidijitali, huku Zanzibar ikiwa ni mandhari nzuri ya sherehe hizi zisizosahaulika za ubora wa Afrika.

Post a Comment

0 Comments