F CMSA yaipongeza TCB kwa kuzinduaTCB Popote Mobile App na kuwa benki ya kwanza nchini | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

CMSA yaipongeza TCB kwa kuzinduaTCB Popote Mobile App na kuwa benki ya kwanza nchini


MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Usimamizi wa Masoko ya Fedha (CMSA),imetoa pongezi kubwa kwa Tanzania Commercial Bank kwa kuwa benki ya kwanza nchini kurahisisha upatikanaji wa hisa kwa njia ya TCB Popote Mobile App.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo CPA. Nicodemus Mkama mapema leo Februari 21, 2025 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya Tanzania Commercial Bank (TCB) na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), ambapo amepongeza ushirikiano huo kwani ni hatua kubwa katika juhudi za kukuza ushiriki wa wananchi kwenye masoko la mitaji na kuimarisha maendeleo ya sekta ya fedha nchini.

“Hatua hii ni sehemu ya mapinduzi makubwa ya kidijitali katika masoko ya mitaji na inakwenda sambamba na juhudi za CMSA na DSE za kuhakikisha ushirikishwaji mpana wa wananchi katika uwekezaji wa soko la hisa.


“Umuhimu wa ushirikiano huu kwa sekta ya Masoko ya  mitaji ni moja ya nyenzo muhimu ya kukuza uchumi wa taifa kwa kuwa yanatoa  fursa kwa mashirika na watu binafsi kuwekeza na kupata fedha za  kukuza biashara zao. Kupitia ushirikiano huu:

“Wananchi wengi zaidi watapata nafasi ya kuwekeza Kupitia teknolojia ya simu ya mkononi, wananchi waliokuwa na changamoto za upatikanaji wa huduma za soko la mitaji sasa wataweza kushiriki kwa urahisi,”amesema.

Ameongeza ongezeko la mtaji kwa makampuni yaliyoorodheshwa kuwa na njia rahisi ya kununua na kuuza hisa kutachochea mahitaji ya hisa na kuongeza uhai wa soko la mitaji.
 
Pia amesema ushiriki wa vijana na wajasiriamali katika uwekezaji teknolojia hiyo inatoa fursa kwa vijana na wafanyabiashara wadogo kuanza safari yao ya uwekezaji mapema kwa mtaji mdogo, hali inayoongeza ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya kifedha.


Amefafanua mfumo huo wa uwekezaji kupitia simu za mkononi utaongeza matumizi ya teknolojia na kusaidia katika mkakati wa taifa wa uchumi wa kidijitali. 

CPA Mkama amesema CMSA inahakikisha kuwa masoko ya mitaji nchini yanaendeshwa kwa uwazi, usawa, na kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya usimamizi wa kifedha na kupitia mfumo huo wa kidijitali wawekezaji watalindwa dhidi ya udanganyifu wa kifedha.

“TCB Popote Mobile App imetengenezwa kwa kuzingatia viwango vya usalama wa kifedha, kuhakikisha kuwa uwekezaji wa wananchi unalindwa.Urahisi wa kupata taarifa za soko la hisa kwa wakati halisiMwekezaji ataweza kufuatilia bei za hisa, mwenendo wa soko, na maamuzi ya uwekezaji bila kutegemea taarifa zisizo rasmi.


“Kuimarika kwa uelewa wa wananchi kuhusu uwekezaji CMSA kwa kushirikiana na DSE na taasisi za kifedha kama TCB, itaendelea kutoa elimu kwa umma ili kuhakikisha wananchi wana uelewa sahihi kuhusu masoko ya mitaji.”

Ametoa rai kwa wananchi wote kutumia fursa hiyo mpya ya kununua na kuuza hisa kupitia TCB Popote Mobile App. Hiyo ni nafasi ya kipekee kwa kila Mtanzania kushiriki katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa njia salama na ya kidijitali.

Amesema Serikali kupitia CMSA itaendelea kushirikiana na wadau wote wa sekta ya mitaji kuhakikisha kuwa masoko yetu yanakuwa imara, yenye uwazi, na yanayowapa wananchi fursa za kuwekeza kwa manufaa yao na kizazi kijacho








 

Post a Comment

0 Comments