MAMALAKA ya Msoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania (CMSA) imezitaka taasisi nyingine kuiga jambo zuri la kufanya tathimini ya utendaji wa masoko ya mitaji kwa mwaka 2024 na matarajio ya mwaka 2025.
Hayo yamebainishwa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA CPA Nicodemas Mkama ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika Hyatt Regency jijini Dar es Salaam
CPA Mkama alisema kitu walichokifanya Vertex ni kikubwa katika ustawi wa sekta ya masoko ya mitaji kuongeza matokeo chanya zaidi hibyo kimatakiwa kuigwa ili kuwa kikubwa zaidi.
"Ni matumaini yangu makubwa mikakati kama hii itaendelea kutekelezwa kwa miaka ijayo ikiimalishwa zaidi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuleta ukuaji katika sekta ya msoko,"amesema Mkama.
Aidha Mkama amesema mwaka 2024 kumekuwa na maendelea makubwa katika uwekezaji uliochochea ubunifu na utoaji wa bidhaa mpya jambo linaloongeza imani kubwa kwa wawekezaji wa ndani na hata nje pia.
Aidha Mkama amesema matumizi makubwa ya teknolojia nayo yamechangia kuongeza mauzo katika soko la hisa, kupitia simu za mikononi zimeongeza ushiriki hasa kwa wawekezaji wa ndani.
Amewataka wadau wote wa masoko ya mitaji kushirikiana vyema na CMSA hasa wakati huu wa mwaka wa fedha kushitikiana katika mikakati kama kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa umma kuhusu fursa na faida zipatikanazo kwenyw uwekezaji.
"Kuongeza idadi ya bidhaa ambapo mamlaka itaendelea kutoa miongozo ya utoaji na usimamizi wa bidhaa na huduma mpya na kuimalisha matumizi ya teknolojia katika kutoa huduma za masoko ya mitaji","amesema Mkama
Kwa upande wa Meneja wa Oparation wa Vertex International Securities Frank Kakweza amesema wameweza kuwafikia Watanzania wengi kuwapa elimu kupitia simu za viganjani.
Kakweza amesema anaamini elimu zaidi ikiendelea kutolewa itawafanya watanzania wengi wazidi kujua nini maana na umuhimu wa soko la hisa.
"Kupitia simu za kiganjani kunamfanya hata mtu wa kijijini ambaye hana uwezo wa kufika katika benki au ofisi zetu anatumia Vertex App, na mpaka sasa watanzania zaidi ya laki 6 wamejioridhesha kwenywe soko la hisa na sisi tunaendelea kutoa elimu zaidi,"alisema Kakwezi
0 Comments