F Gekul aanza kufunga mahesabu,amsifu Rais Samia kwa Maendeleo Babati. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Gekul aanza kufunga mahesabu,amsifu Rais Samia kwa Maendeleo Babati.

Na John Walter -Babati

Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul, ameanza kufunga mahesabu ya miaka mitano ya uwakilishi wake, akieleza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hana deni kwa wananchi wa Babati kutokana na miradi mingi ya maendeleo iliyotekelezwa.

Akizungumza na wananchi wa Himiti, Gekul aliwahakikishia kuwa Jimbo la Babati lipo salama, huku akitaja miradi mikubwa iliyotekelezwa na serikali, ikiwemo:

✅ Ujenzi wa Wodi ya Wanawake katika Hospitali ya Mji wa Babati kwa gharama ya Shilingi milioni 500.


✅ Shule ya Wasichana Manyara iliyoyopo Mjini Babati ambayo imejengwa kwa zaidi ya Bilioni 3, kuongeza vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, ikiwa ni pamoja na CT Scan.


✅ Ujenzi wa Zahanati, Kituo cha Afya na Jengo la Watoto Njiti.


✅ Uwanja wa kisasa wa mpira Tanzanite Kwarara.


✅ Bilioni 17 zimetengwa kwa ujenzi wa Stendi Kuu ya Babati na barabara ya kilomita 10 za lami, ujenzi unaotarajiwa kuanza Mei 2025.

Wananchi wa Himiti, Kata ya Bonga, wameeleza kuwa hawana cha kumdai Gekul kutokana na maendeleo makubwa aliyoyasababisha katika kijiji chao.

 Wamesema wanasubiri muda ufike ili wamlipe kwa kura kutokana na kazi kubwa aliyoifanya.

Diwani wa Kata ya Bonga, Hiiti Qambalal, amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amewaheshimisha na kuwaondolea maswali viongozi wa eneo hilo kwa kuwapatia fedha nyingi za miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa Shule ya Sekondari Gekul iliyopo kijijini Himiti.

Mbunge huyo amewashukuru wananchi wa Babati Mjini, wenye idadi ya wapiga kura zaidi ya 8,000, kwa kumuamini na kushirikiana naye katika kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi.

Amesisitiza kuwa ni muhimu wananchi waendelee kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumpigia kura ifikapo Oktoba 2025 ili aendelee kuongoza kwa miaka mingine mitano.

Pia, ameeleza kuwa Rais Samia amekataa rushwa katika uchaguzi, akisisitiza kuwa maendeleo ya Tanzania hayawezi kusimama kwa sababu ya siasa zisizo na tija.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Abdulrahaman Kololi, amesema kuwa maendeleo yanayoonekana katika jimbo hilo ni matokeo ya juhudi kubwa za Gekul, akisisitiza kuwa Babati imependeza zaidi chini ya uongozi wake.

Post a Comment

0 Comments