F Shule ya Sekondari Manyara Boys inajengwa kwa kasi. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Shule ya Sekondari Manyara Boys inajengwa kwa kasi.


Na John Walter -Babati

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Manyara Boys, inayojengwa katika Kijiji cha Ngoley, Kata ya Mwada.

Shule hiyo inajengwa na Serikali kupitia Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) na inatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi bilioni 4.1 hadi kukamilika kwake.

Wakati wa ziara hiyo, timu hiyo ilitoa msisitizo kwa mafundi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa wakati na kuzingatia viwango vya ubora vinavyotakiwa.

Aidha, walihimiza kuongeza nguvu ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa ufanisi na kwa mujibu wa mpango wa serikali wa kuboresha elimu nchini.

Shule ya Sekondari ya Manyara Boys inatarajiwa kuwa miongoni mwa shule muhimu za kanda ya kaskazini, ambapo baada ya kukamilika, itapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi kidato cha sita kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Ujenzi wa shule hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuongeza fursa za elimu na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa vijana.

Wakazi wa eneo hilo na wadau wa elimu wanatarajia shule hiyo itakuwa na mchango mkubwa katika kuinua kiwango cha elimu katika mkoa wa Manyara na kanda ya kaskazini kwa ujumla.
 

Post a Comment

0 Comments