WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Khalid Salum Mohamed amewapongeza Vertex International Securities kwa kuanzisha dawati la uwekezaji kupitia Shirika la Posta Tanzania.
Rai hiyo ameitoa hii leo katika hafla ya uzinduzi wa dawati hilo uliofanyika Serena Jijini hapa, akiamini ni hatua kubwa hasa kuona taasisi binafsi zikishirikiana na Serikali kufanya jambo jema na la kuigwa kama hilo.
"Huduma za kifedha naamini zitawafikia wengi waliokosa fulsa za kushuriki katika masoko ya mitaji na hilo ndilo lengo kubwa ambalo Vertex wameliwaza na kulitekekeza nawapongeza sana kwa maono yenu ya kuwafikia wananchi kwa wepesi,"amesema.
"Huduma hii ya dawati la uwekezaji itawapatia fulsa kuhusu uwezekaji na umuhimu katika kuboresha maisha ya kila siku, na sisi kama Serikali tunajitahidi kuona uchumi jumuishi kwa kila mtanzania akishiriii kimamilifu,"
Mohamed amesema, wananchi fedha wanazo akitolea mfano kule Zanzibar wavuvi wanapesa nyingi lakini shida ni kuziongoza pesa hizo ndio kazi kubwa ambayo inawakabili hivyo wakipewa elimu watabadilika.
"Uwekezaji wa kuingia soko la Mitaji hauna athari yoyote tuwasaidie wananchi kiwapa elimu ili wajue pesa zao zitakuwa salama, wengi hawajui kabisa kuhusu haya mambo,"anasema Mohamed.
Amesema mambo ya kifedha yanahitaji sana ubunifu hivyo anatarajia kuona matokeo chanya ambayo yatasaidia wananchi kujua vyema juu ya uwekezaji na kulitumia vyema dawati hilo.
"Shirika la Posta lipo katika mikono salama naamini kupitia hili tutaona makubwa sana, faida za dawati la uwekezaji ni kubwa sana hivyo kila mwananchi anayo nafasi ya kushiriki kujenga uchumi shirikishi endelevu na sasa ni kidigitali zaidi,"amesema Mohamed.
"Dawati hili litawapa wepesi wananchi kupata magawio ya hati fungani na mambo lukuki naamini ushirikiano huu utaimalisha mapato Posta na pia kuboresha miundombinu kwa kuwa kutakuwa na shughuli zinafanyika muda wote,"amesisitiza.
Mkurugenzi mtendaji wa Vertex International Securities Mateja Mgeta amesema, huduma hiyo ni ushirikiano kati ya Vertrx na Shirika la Posta ikiwa na lengo ni kuboresha upatikanaji wa soko la mitaji nchini Tanzania, hata hivyo bado tunakabiliwa na pengo la ushiriki wa umma katika uwekezaji wa mitaji.
"Pengo linatokana na imani potofu kuhusu uwekezaji, utakuta wanasema kuwekeza katika hisa ni suala la matajili wakati kiasi cha uwekezaji nikidogo, changangamoto kubwa ni elimu ikitolewa suala la uchumi wezeshi litakuwa kubwa"amesema Mgeta.
Amesema sababu za Vertex kufanya kazi na Shirika la Posta ni kuweza kuwafikia haraka kwa kuwa Posta wana matawi zaidi ya 500 hapa nchini hivyo itakuwa vyepesi kuwafikia wengi nchini.
"Lengo letu lina sura kuu mbili kuwapa maarifa na maamuzi sahihi ya kufanya uwekezaji, tunaamini elimu ndio itakuwa ufunguo wa hili, na pia tunapenda huu nchakato uwe mwepesi na rahisi,"
Amesema masoko ya mitaji yanajukumu muhimu ya kukusanya na kuendeleza ajira kwa watu wengi na pia kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa Taifa.
"Tupunguze utegemezi kutoka nje nawashukuru shirika la Posta kwa kukubali kuwa mshirika muhimu kwetu katika kukamilisha hili, tunawashukuru CMSA, DSE kuweka njia nyepesi za kufanya uwekezaji kuwekeza ni jukumu letu kuhakikisha elimu inawafikia.
''Uzinduzi wa leo ni mwanzo tutaanzisha vituo vingi vya mawasiliano katika ofis za Posta ili kuwafikia kwa wepesi wananchi wengi waweze kuwekeza"amesisitiza Mgeta.
Kwa upande wa Posta Masta Daniel Mbodo amesema wamejipanga kuhakikisha huduma hii inawafikia vyema wananchi na kufanya uwekezaji kupitia vituo mbalimbali ya Posta.
"Dawati la uwekezaji litapatikana ofisi zetu zote nchini huduma ya kuuza na kununua hisa itakuwa inapatikana,"amesema.
Leonald Kameta mwakilishi kutoka Soko la hisa Dar es Salaam (DSE) amesema, ni hatua kubwa katika kuimarisha soko la hisa la Dar es Salaam na idadi ya ongezeko la wawekezaji limekuwa kubwa.
"Tunawaona kupitia DSE kiganjani kwa siku watu 200 wanaongezeka na umri wao ni vijana miaka 29 hadi 40 jambo ambalo linatufanya kujivunia na tukio hili la leo linaongeza chachu kwa wawekezaji, na pia ni jukumu letu kuhakikisha watanzania wanaishi sehemu ya ukuaji jumuishi kwa pamoja kwa ubunifu huu wa Vertex unaleta matumaini mapya"amesema.
0 Comments