Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chumba cha kuhudumia wakina mama na Watoto wakati wa kazi, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, amesema mpango huo ni muhimu katika kuchochea utekelezaji wa sera za ujumuishi wa kijinsia kwenye eneo la kazi na kuweka mazingra rafiki kwa wazazi kuhudumia vichanga vyao wawapo kazini.
“Thamani ya Airtel Tanzania inatokana na hulka yetu ya kutenda kile tunachokisema. Tunahakikisha kila mabadliko tunayoyazungumzia tunayatekeleza. Chumba hicho cha kuhudumia wakina mama na Watoto wakati wa kazi kinahakisi jitihada zetu endelevu za kuwaunga mkono wanawake.
Tunawawezesha Airtel Divas to kusonga mbele kwenye kazi zao na maisha yao binafsi bila ya kuchagua kati ya kulea uzazi na ajira,” alisema Kamoto.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Rasilimali Watu, Stella Kibacha alifafanua kuwa mpango huo unahakisi dhumuni la dhati la Airtel Tanzania kutengeneza eneo la kazi ambapo wanawake wanaweza kupata maendeleo kwa kuwa chumba hicho kitaboresha maisha ya wakina mama ambao wanafanyakazi.
“Eneo hili ni mahususi kuhakikisha wakinamama wanaweka usawa kati ya kazi na majukumu binafsi kwa uadilifu na wepesi. Tunawaunga mkono wakina mama kwasababu kufanya hivi kutaboresha maisha yao wakiwa kazini pamoja na kuboresha uzalishaji wao,” alisema.
Akizungumzia uzinduzi wa chumba hicho, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adrianna Lyamba alisema kuwa mpango huo ni muhimu kwasababu inawafanya wakina mama wafanyakazi wawe na saikolojia chanya.
“Majukumu ya uzazi hayapaswi kuwa kikwazo kwa mtu kupanda ngazi kwenye eneo lake la ajira. Tunaelewa kuna changamoto zinazoambatana uzazi wakati wa kutekeleza majukumu ya kikazi, jambo ambalo linaweka msisitizo juu ya umuhimu wa uwepo wa chumba kwa ajili ya wakina mama kuhudumia watoto wao wanapokuwa kwenye eneo la kazi.
Uwepo wa chumba hicho kinawapa wanawake utulivu wa kiakili kwasababu wanatambua kuwa kuna chumba maalum watakachotumia kulea vichanga vyao huku wakiendelea na kazi. Mpango huu ni msisitizo kuwa Airtel inaendelea kuchochea hatua zitakazohakikisha wanawake wanaungwa mkono kwenye kila nyanja,” alisema Lyamba.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Ugavi wa Airtel Tanzania, Daniel Akuffo, alisema kuwa chumba hicho kipya kinaonyesha azma ya Airtel katika maono yake mapana ya ujumuishi na uwezeshaji.
“Ukizungumzia eneo la kazi lenye mazingira wezeshi, maana yake ni kutengeneza mazingira ambayo yatamfanya kila mfanyakazi aweze kukua kitaaluma na katika maisha yake binafsi.
Uzinduzi wa chumba hiki inaonyesha dhamira yetu ya kutengeneza eneo la kazi lililojumuishi. Wafanyakazi wanapoona wanaungwa mkono, wanakuwa na ari na ufanisi zaidi hali inayowanufaisha wao pamoja na kampuni kwa ujumla. Tunamatumaini kuwa mpango huu utaweka kiwango kwa ajili ya makampuni ya Tanzania na kuhamasisha makampuni mengine kutekeleza sera kama hizi.”
0 Comments