Na Ahmad Mmow, Lindi.
Bodi ya Korosho Tanzania (Cashewnuts Board of Tanzania ( CBT) imedhamiria kumaliza changamoto ya mashamba pori ya mikorosho nchini ili kuongeza uzalishaji wa korosho.
Hayo yameelezwa leo na mkurugenzi mkuu wa CBT, Fransi Alfred wakati wa hafla ya uzinduzi wa kukabidhi vitendea kazi kwa maofisa ugani 152 waliopo mkoani Lindi. Hafla ambayo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi iliyopo katika manispaa ya Lindi.
Alfred amesema kwa msimu huu wa 2025/26 lengo ni kufikia tani laki saba, na hadi kufikia mwaka 2030 inatarajiwa kufikia tani milioni moja. Lengo ikiwa ni kuleta mabadiliko na kila mkulima afikiwe na huduma za ugani. Ambapo maofisa licha kuhakikisha uzalishaji unaongezeka, lakini pia watasaidia kufufua mashamba pori.
Amesema maofisa ugani hao ambao wameajiriwa na CBT wamepewa elimu juu ya kutibu magonjwa lakini pia watakwenda kusaidia uzalishaji wa mazao mengine na shughuli zingine husika.
Anesema watashugulikia pia zoezi la kupokea na kugawa pembejeo za kilimo. Lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu ili kila mkulima afikiwe na afisa ugani.
" Kwa msimu huu wa 2025/2026 tunalengo la kufikia uzalishaji wa tani laki saba. Na hadi kufikia mwaka 2030 tunarajia kufikia tani milioni moja. Lengo ni kuleta mabadiliko ili kila mkulima afikiwe na huduma za ugani," alisema Alfred.
Aidha mkurugenzi mkuu huyo wa CBT alibainisha kwamba maofisa ugani hao pia watasimamia ugawaji wa pembeje kuanzia katika vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) hadi wakati wa mauzo kwenye maghala.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Zainab Telack ambae alikabdhi vishikwambi na pikipiki kwa maofisa ugani 152 amewataka wakatumie vitendea kazi hivyo kwa kazi zilizokusudiwa. Huku akionya vitumiwe na watu wasio maofisa ugani.
Nao baadhi ya maofisa ugani hao, Steven Osward na Winfrida Mashala wamesema wapotayari kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kufikia lengo la uzalishaji linalokusudiwa. Huku wakiahidi kutumia vitendea kazi hivyo kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
Katika uzinduzi huo maofisa ugani 152 walikabidiwa pikipiki na kishikwambi(tablet) kila mmoja. Vifaa ambavyo vimetolewa na CBT. Ambapo mkuu wa mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Zainab Telack alikabidhi kwa wataalamu hao.
0 Comments