F KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA TRC KWA TRENI YA MWENDO KASI SGR | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA TRC KWA TRENI YA MWENDO KASI SGR


NA REBECA DUWE TANGA

KAMATI ya kudumu  ya bunge ya Miundombinu imelipongeza Shirika la Reli Nchini 'TRC' kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Reli ya Kisasa 'SGR', Pamoja na maboresho ya Miundombinu ya Shirika hilo huku Kamati hiyo
ikiitaka Mamlaka ya Bandari Nchini  'TPA' pamoja na shirika la Reli 'TRC' kuanza kutekeleza mpango wake  wa  kuunganjisha njia ya Reli na Bandari ya Tanga  ambapo kukamilika kwake linatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa ndani na nje ya nchi.

Maagizo hayo yametolewa na kamati hiyo kupitia kwa mwenyekiti wake Suleiman Kakoso  wakati walipofanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya upanuzi wa bandari , uwanja wa ndege pamoja na maboresho ya Reli iliyopo Mkoani hapa ambapo  wameipongeza Serikali kupitia maboresho yanayofanyika katika miradi hiyo.

"Tumefurahishwa na mipango ya baadaye ambayo sasa mamlaka ya bandari nafikiria kwenda mbali zaidi muanze kuweka mifumo  ya kuunganjisha  Reli na Bandari ili tugwe na miradi mikubwa"

Aidha ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya ujenzi na uchukuzi ambayo imeanza michakato ya ujenzi wa Reli za Kisasa katika maeneo mbalimbali nchini ambayo utakapo kamilika itafungua fursa mbalimbali ikiwemo za kiuchumi.

"Kitendo cha kuanza kufikiria kujenga Reli za Kisasa Mikoani itasaidia sana kuongeza mzunguko wa fedha kwa Wananchi wetu,tunashauri  Serikali iwe inashirikisha wawekezaji  katika ujenzi wake" alisema Kakoso

"Pamoja na uwekezaji mkubwa ambao mnaweka kwenye  kwenye Shirika la Reli,Bunge linashauri ni vyema uwekezaji wenu uende sawa na  vitendea kazi ili uwekezaji uwe na tija" alisema.

Alisema mkoa wa Tanga unaendelea kufunguka kupitia fursa mbalimbali ikiwemo za kiuchumi katika utekelezaji wa miradi mikubwa kama  ujenzi wa Barabara, ukarabati wa Reli  samabama na ujenzi wa Barabara  ya Tanga hadi Singida pamoja na Ile ya Tanga hadi Bagamoyo.

Kwa upande wake  Kaimu Mkurugenzi uendeshaji kutoka shirika la Reli Tanzania 'TRC' Focus Sahani ameeleza  kuwa  wameendelea kuhakikisha usafiri wa njia hiyo unaimarika ambapo hadi kufikia sasa Kila wiki wa siku nne wanayoa huduma ya safari za Treni za abiria kutoka Dar es salaam,Korogwe Moshi na  Arusha.

"Tumepata pongezi kubwa sana kuhusu uanzishwaji wa Treni ya kisasa ya SGR pamoja  hiyo lakini tuna Treni yetu ya MGR tunatoa huduma ya Tren ya abiria katika mikoa ya Kanda ya kaskazini Kila wiki tuna safari nne za Treni tangu tulipoifungua hiyo Reli, Kila  tunapofika kuanzia mwezi November mpaka February  huwa tunaong za Treni zinakuwa  sita kwa wiki kwaajili ya kuwahudumia watanzania" alisema  Sahani.

Alisema Shirika linaendelea na kazi ya kuzifungua Reli zinazoelekea katika bandari ya Tanga ambapo  kazi iliyopo ni kubadilisha miundombinu iliyopo kutokana na uchakavu wake ambapo Serikali imetoa fedha kwaajili ya ujenzi huo.

"Kwa hapa Tanga bado tunaendelea kufungua hizo Reli kwaajili ya kwenda bandarini kilichobakia sasa ni kuboresha  njia za Reli karibu na eneo la bahari  juhudi zinaendelea kufanyiwa kwa sababu Reli hizo zimechakaa na Serikali sasa imeshayoa fedha  kwaajili ya kupata vifaa vya ujenzi huo"

Akizungumzia  juu maendeleo ya  mradi wa Reli ya kisasa 'SGR' Sahani amesema kuwa baada ya kukamilika kwake na kufanyiwa majaribio na hatimaye kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan tayari mpaka  zipo Treni 8 za abiria zinazotoa huduma ya safari za abiria kutoka Dar es salaam hadi Dodoma.

" TRC baada ya kupewa mamlaka ya kusimamia  Reli tulianza na ujenzi  ya SGR'  kilichofuata ni uendeshaji wa Tren ambapo tulianza kwenye majaribio kuanzia Dar es salaam kwenda Morogoro, lengo  likiwa ni kufika  Dodoma baadaye tulianza majaribio ya kwenda Dodoma  tukaanza oparesheni na mpaka  sasa tuna safari 8 za Treni kwenda Dodoma  maana yake Dar es salaam na Dodoma sasa hivi imekuwa ni karibu" alisema.

Post a Comment

0 Comments