Na John Walter -Babati
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Paul Mnzava, ameongoza Wajumbe wa Kamati hiyo kukagua Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Iliyotengewa Fedha kwa Mwaka wa Fedha wa 2024/2025 katika mkoa wa Manyara.
Katika Ziara hiyo iliyoanza tarehe 12 Machi, 2025, Kamati imetembelea na kukagua Mradi wa Programu ya Kupanga, Kupima, na Kumilikisha Ardhi katika Halmashauri ya Mji ya Babati pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Lango la Kuingia Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kutokea Babati (Lango la Mamire) na Ujenzi wa barabara katika hifadhi hiyo.
Kamati hiyo ilipokelewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geofrey Pinda (Mb) pamoja na uongozi wa Mkoa wa Manyara.
Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii inafanyika ikiwa ni sehemu ya utendaji wa shughuli za Kamati za Bunge katika kukagua utekelezaji wa miradi ililiyotengewa Fedha kwa 2024/2025 kwa mujibu wa Kanuni ya 117(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023.
0 Comments