NA REBECA DUWE TANGA
MKUU wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani ameeleza miradi mikubwa ikiwemo Bandari uliogharimu Bilion 429 Ambayo ilitembelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samaia Suluhu Hassan alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi mikoani Tanga .
Akizungumza na waandishi w habari ofisini kwake alisema kuwa ujio Rais Dkt Samia umeweza kufumbua mazuri mengi kwa wakazi wa mkoa wa Tanga kwani wengi walikuwa wanatamani wangesikia samaiaazungumze na wananchi na kusikia kutoka kwa mama Samia.
Aidha kwa Mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian alisema kuwa mnamo tarehe 22 feburary mwaka huu ndio Mh.Rais Dkt Samia kuanza ziara Yake kuazindua Hjospitali ya wilaya Handeni ambapo wananchi wengi waliojitokeza na kumsikiliza Dk mama Samia kwa kazi kubwa iliyofanya a serikali yake.
Alisema kuwa watu wengi waliojitokeza wakiwemo wafanya biashara, bodaboda, viongozi wa dini,wasanii Kinamama wa Tanga ambapo walimpokea kwa baibui la ukaya na hivyo hivyo imani ya wanatanga imekuwa kubwa kwake kwa ushirikiano waliouonyesha.
Mkuu wa mkoa Tanga alieleza miradi Michache ambayo Mama samia alitembelea na kuzindua ndani wilaya za mkoa wa Tanga,ambayo imegharimu trillion 1 na milioni Mia nane , ikiwemo mradi wa jengo la utawala Bumbuli wilaya Lushoto jengo la utawala Handeni Mji.
Sambamba na hayo Balozi Buriani alisema Dkt. Samai alizindua mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika wilaya ya Korogwe ambao uligharimu sh. bilioni 18. lego kuu ni wakazi wa Korogwe ambao ni wakulima mpungu kunufaika na kuongeza tija.
"Mradi shule ya Sayansi ya umahiri ya wasichana katika Wilaya ya Kilindi mkoani humo ambapo serikali ya awamu ya Sita imedhamiria kuboresha elimu kwa wasichana lakini pia itainua wilaya yetu kilindi kwani hata huduma muhimu serikali ishaanza kupeleka maji ikiwemo huduma ya Maji ambapo wakala wa maji vijijini Ruwasa wamepeleka maji lakini pia kuna mpango uliowekwa tayari wankuleta maji Mvomero .,"
Mradi mwingine ni Barabara ya Tanga Pangani Saadani bagamoyo ambao inaruti tatu ambapo ruti ya kwanza bilioni 98 ruti ya ya pili biioni 92 ruti Tatu bilioni 94 hivyo inaweza kusaidia kwenda kuondoa changamoto ya usafiri kwa watanzania kwani hata wananchi wa pangani walikuwa wanatumia Pantoni lakini daraja linaanza kukamilika. " Ameeleza mkuu wa mkoa Tanga Blozi Buriani.
Ambao miradi ya maji serikali ya Samia imeleta mradi miji 28 ambao unasimamiwa naTanga uwasa , lakini pia mkinga kuna mradi maji ambao maji yake yanatoka mto zigi,katika wilaya Handeni maji ya msitu wa Bondo ambao unapeleka maji kwenye mto zigi .
Aidha kutokana mradi huo maji pia miongoni wanufaika ni wanafunzi wa shule ya sayansi ya wasichana wilaya ya kilindi ambao tayari wamepata maji safi na salama.
sambamba na hilo Rais Samia aligawa mtingu ya gesi elfu 21 ,ambapo ni ugawagiji wa majiko ya ruzuku ambayo imeuzwa kwa sh.17000, hivyo serikali imezingatia kujali mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchi lengo kuu ikiwa ni kuhamasisha nishati safi.
Mkuu wa mkoa w Tanga alielezea kuwa Kampuni ya mafuta ya GBP ambayo inazalisha Lita milioni 200 ambayo ilikuwa imekusudiwa kusaidia mikoa ya kaskazini yatumia Tanga iii kuweza kutekeleza agizo la serikali lakini Sasa Kampuni hiyo imefanya uwekezaji wa gasi ambayo itauw na uzalizaji mkubwa wa mara mbili zaidi makumpuni yote yanayotengeneza gasi.
0 Comments