Katika miaka minne ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, wilaya ya Mkinga katika Sekta ya Maji imeidhinishiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 47.
Haya yamebainika wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mkinga Mhe. Dunstan Kitandula akizindua Mradi wa Maji Vuga-Kigongoi uliopo katika kata ya kigongoi kijiji cha Vuga ambao unagharimu zaidi ya Shilingi milioni 195 na unaenda kunufaisha wananchi 1573.
Katika hotuba yake Mhe. Kitandula alisema kuwa Mtangulizi wake katika kiti cha Ubunge Mhe. Mbaruk Kassim Mwandoro moja ya nasaha alizompa akimkabidhi kijiti cha kuwa Mbunge alimuachia changamoto kubwa mbili azishughulikie na kuzipa umuhimu mkubwa ni suala la Maji na Elimu.
Mhe. Kitandula aliongeza kuwa changamoto ya Maji katika wilaya Mkinga inaenda kuwa jambo la historia ya kale kufuatia utekelezwaji wa miradi unaoendelea kwa sasa chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan. Mhe. Kitandula anasema ushughulikiaji wa changamoto ya Maji imekuwa kipaumbele chake tangu awe mbunge, akiainisha miradi ya Maji katika kata za Daluni, Mapatano, Doda, Parungu Kasera, Duga Sigaya, na Duga ambayo yote utekelezaji wake umefanyika katika kipindi cha uongozi wake.
Vilevile Mhe. Kitandula alisema tatizo la maji katika eneo la ukanda wa Pwani linaenda kupatiwa suluhisho la kudumu kupitia mradi mkubwa wa Maji kutoka moto Zigi hadi Horohoro, ambao utawezesha upatikanaji wa Maji kufikia zaidi ya asilimia 85 katika vijiji vya wilaya MKINGA.
Mradi wa Maji wa kutoka Mto Zigi hadi Horohoro ambao utahudumia vijiji 37 unaenda kuleta suluhisho la kiafya, na kuifungua Mkinga kiuchumi kupitia fursa za kiuchumi zilizopo ambazo hapo awali ilikuwa vigumu kwa wawekezaji kujitokeza kutokana na changamoto ya kutokuwepo Maji ya uhakika.
Akizindua Mradi Vuga, Mhe. Kitandula aliongeza kuwa utekelezaji wa Ilani ya CCM katika wilaya ya Mkinga imetimizanakwenda vizuri chini ya Jemedari Mwenyekiti wa Chama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alisema hili la kumtua mama wa Vuga ndoo kichwani kwa kuwa kinamama wa Kijiji cha Vuga na Vitongoji vyake ni uthibitisho tosha kuwa CCM imedhamiria kuwaletea wananchi Maendeleo kwa kutatua kero zinazowasumbua; na kwamba wanavuga hawatalazimika kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta Maji.
Katika Hatua nyingine Katibu Tawala wa Wilaya Mkinga Ndugu Palango Salumu alimshukuru Naibu Waziri na Mbunge wa Mkinga kwa kuwa mstari wa Mbele katika kuhakikisha wilaya inapata maendeleo stahiki.
Ndugu Palango akiwa ameongozana na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Mkinga aliwataka wananchi wa kata ya Kigongoi na maeneo mengine kuitunza Misitu ya iliyoko maeneo hayo kwakuwa ni chanzo kikubwa.
0 Comments