Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe ambaye ni diwani wa kata ya Utalingolo Erasto Mpete amejumuika pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislam kwenye Sala ya Eid Al Fitr katika Msikiti wa Madina uliopo Idundilanga mjini Njombe leo March 3,2025.
Mpete ametumia abada hiyo kutoa wito kwa watanzania kuendelea kudumisha amani.
"Nimekuja hapa kwasababu wote ni watanzania na tudumishe amani na kudumisha amani ni kama hivi tulivyokutana katika ibada na kushirikiana"amesema Mpete
Kwa upande wake Shekhe wa Mkoa wa Njombe Rajab Msigwa ametoa wito kuyaenzi mafundisho yaliyotolewa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani hata baada ya kumaliza funga.
"Tumekuwa wenye nidhamu sana katika mwezi mtukufu wa Ramadhani nidhamu hii ndio mafundisho ambayo Mwenyezi Mungu anatuhitaji tuishi nayo katika miezi kumi na moja inayokuja kwa hiyo sote tukizingatia mafunzo haya tutaendelea kuishi vizuri"amesema Msigwa
Siku kuu za Eid el Fitir husherekewa baada ya kutamatika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani katika kipindi cha mwezi mmoja mara baada ya mwezi kuandama.
0 Comments