F Mwenyekiti wa BAWACHA Manyara awaasa Wananchi Kuchangia CHADEMA Kupitia Mfumo wa Kidijitali | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mwenyekiti wa BAWACHA Manyara awaasa Wananchi Kuchangia CHADEMA Kupitia Mfumo wa Kidijitali

Na John Walter -Hanang 

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Manyara, Regula Mtei, ametoa wito kwa wanachama na wananchi wanaokitakia mema chama hicho kuchangia kupitia mfumo wa kidijitali uliozinduliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Mfumo huo wa kuchangia unafanyika kupitia kampeni za ‘Tone Tone’ na ‘Tone Nimo’, ambazo zinalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kufanikisha kampeni ya ‘No Reforms, No Election’. Kampeni hiyo ilipitishwa katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA uliofanyika Januari 21, 2025, kwa lengo la kushinikiza mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi ili kuwezesha chaguzi huru na za haki nchini.

Mtei akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani ya Chama hicho wilayani Hanang', amesisitiza kuwa fedha zitakazokusanywa zitatumika kugharamia mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali, hususan vijijini, kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa mageuzi ya mfumo wa uchaguzi.

"Kama tunataka uchaguzi wa haki, lazima tushiriki kwa vitendo, Njia mojawapo ni kuchangia kampeni hii kupitia mifumo iliyowekwa," alisema Mtei, akihimiza kila mwananchi mwenye mapenzi mema na demokrasia kuunga mkono juhudi hizo.

Kampeni hii itadumu kwa miezi sita, na lengo la awali ni kukusanya Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kufanikisha harakati hizo.

Post a Comment

0 Comments