F RC Manyara atoa wito kwa Viongozi Kuhusu Uwajibikaji. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

RC Manyara atoa wito kwa Viongozi Kuhusu Uwajibikaji.

Na John Walter -Hanang' 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amewataka wenyeviti na watendaji wa mitaa, vijiji na vitongoji kuhakikisha wanawapatia wananchi taarifa sahihi kuhusu mapato na matumizi katika maeneo yao. Pia, amesisitiza kuwa ni wajibu wa viongozi hao kuwafahamisha wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayofanywa na serikali ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo.

Akizungumza akiwa wilayani Hanang’, ambako anafanya ziara ya kikazi ya siku nne kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi, Sendiga aliagiza kuwa kila mwananchi anapaswa kupata taarifa kuhusu matumizi ya rasilimali za umma.

Aidha, amemuagiza Mkuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa wananchi wanapokea taarifa muhimu zinazohusu miradi inayotekelezwa na serikali, ili waweze kufuatilia maendeleo na kutoa maoni yao kwa uwazi.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wilayani Hanang’ inalenga kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na wananchi wananufaika na huduma zinazotolewa na serikali.

Post a Comment

0 Comments