Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani ameeleza kuwa zaidi ya shilingi Trillion 1.2 zimeenda kwenda sekta ya maji katika mkoa wa Tanga ambayo ni fedha iliyotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuondoa changamoto ya ukosefu wa maji kwa wananchi wa mkoa Tanga.
Balozi Dkt.Batilda aliyasema hayo wakati akizindua program ya kitaifa ya visima 900 inayolenga kuhakikisha zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wa maeneo ya vijijini kupata huduma ya maji safi na salama na kutimiza azma ya serikali ya kumtua mama ndoo kichwani.
Aidha Balozi Dkt. Batilda alizindua mradi huo katika kijiji cha Makorora kata ya Magoma wilaya Korogwe ikiwa na lengo mradi huo ni kutekeleza azma serikali ya kuondoa changamoto ya majikwa wananchi ambapo mapa Sasa wilaya ya Korogwe inanufaika na mradi huo katika vijiji vya Mwakinyumbi Station Makorora kwaisewa,Makoya ,Buiko,Ngombezi na kilole kwa mzee.
Akisoma taarifa ya mradi Meneja wa wakala wa maji vijijini Ruwasa Wilaya Korogwe Injinia Muharami Mohamed alisema mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milion 656,472,450 kupitia fedha za Lipa kwa matokeo (pay for R na national fund.).
Mradi wa uchimbaji wa visima umekamalika kwa alisimia 100 ambapo ujenzi wa visima umekamilimika kwa asilimia 85 kwa ajili ya kutekeleza azma ya serikali ya kuondoa changamoto ya ukosefu wa maji vijijini vya Mwakinyumbi Station, Makorora Kwaisewa, Makoya, Buiko Ngombezi,Kilole kwa mzee na Mgambo.
Lengo la serikali katika wilaya ni kufikia wanannchi wapatao 9450 ambapo kwa Sasa upatikanaji wa maji umeongezekq hadi kufikia asiliamia 69.9 alikini ujenzi huo wa visima vya maji umeweza kunufaisha wananchi wapatao 50 kupata ajira ya mud mfupi
Kwa upande wake Meneja wa wakala wa maji vijijini Ruwasa Injinia Upendo Lugongo aliwaadi wananchi wananchi wote kufikiwa na huduma za majivkupitia mtandao huo ndani ya muda mfupi kwamba watu wote watakunywa na kuoga maji safi na salama
0 Comments