F Sillo akabidhi mashine ya kutoa copy Duru Sekondari. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Sillo akabidhi mashine ya kutoa copy Duru Sekondari.


Na John Walter -Babati 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Mheshimiwa Daniel Baran Sillo, ameendelea kutimiza ahadi zake kwa wananchi kwa kukabidhi mashine ya kushapishia na kutoa nakala (photocopy machine) katika Shule ya Sekondari Duru.

Akikabidhi mashine hiyo, Mheshimiwa Sillo amepsema kuwa amekuwa akitoa mashine za kuchapisha mitihani katika shule mbalimbali za sekondari na msingi ndani ya jimbo lake, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya elimu na kuongeza ari ya ufaulu miongoni mwa wanafunzi.

Kwa upande wake, Katibu wa Bodi ya Shule ya Sekondari Duru, Lucas Qwaray,akisoma taarifa kwa niaba ya shule, ameeleza kuwa msaada huo utasaidia kuzalisha mitihani kwa urahisi zaidi na kupunguza gharama ambazo shule ilikuwa inatumia awali kwa uchapishaji wa mitihani.

Aidha, imeelezwa kuwa mashine hizo zinazotolewa na Mheshimiwa Sillo katika shule mbalimbali zinatokana na fedha za mshahara wake, hatua inayoonyesha dhamira yake ya dhati katika kuinua kiwango cha elimu katika jimbo la Babati Vijijini.

Walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Duru wameelezea furaha yao na kumshukuru Mheshimiwa Sillo kwa msaada huo, wakisema kuwa utawasaidia sana katika urahisi wa maandalizi ya mitihani na nyaraka nyingine muhimu za shule.


Picha mbalimbali ziara ya Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Mheshimiwa Daniel Sillo shule ya Sekondari Duru.


















Post a Comment

0 Comments