NAREBECA DUWE, TANGA.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian ametoa wito kwa Jumia za watumia maji mkoa wa Tanga ufanya kazi kwa uadilifu na weledi ili kuhakikisha wananchi wanapata maji kama ambavyo serikali imekusudia ya kumtua mama ndoo kichwani.
Hayo aliyasema wakati akifungua mafunzo ya siku 7 ya wasimamizi wa vyombo vya usimamizi wa utoaji huduma za maji vijijini CBWSO iliyofanyika katika Halmashauri ya wilaya korongwe mkoani Tanga.
Aidha alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama hivyo ni vyema kuwa wakali ili timu yao ifanye kazi kwa uadilifu na weledi
bila kumuuza mwananchi wa kawaida maji yasifungwe bila ya kuwa na sababu.
Aliongeza kusema wanapaswa kupanga bei kwa mpango shirikishi na watoa maji binafsi ili kuhakikisha huduma za maji zinafika kwa kila mtu Lakin maji yasitoke kwa mtu binafsi tu na kwenye mabomba yenu yasitoke
"Nawapon.geza kwa ongezeko la ukusanyaji wa pesa kwa kutoka mlioni 58 ya kwa mwaka Jana mpaka kufikia milioni 141 mbayo ni sawa na asilimia 140.lakini
kwa fedha wa 2024 /2025 shilingi bilioni 1na milion120 zimetuka ambayo asilimia 98 ya makusanyo ya ndani."alisema Buriani.
Kwa upande wake meneja wa Ruwasa alisema mafunzo ni ya kuhakikisha miradi ya maji inakuwa endelefu lakini pia na bajeti ambayo itaakisi kuwa miradi itakuwa endelevu na itakuwa na mafunzo na kazi lengo kuu ikiwa huduma ya maji katika vijiji vote vya Tanzania.
Lengo kubwa washiriki wanaenda kuwa watoaji wa mafunzo kwa wasimamizi wengine ambao hawjafika ili kuimarisha na kuboresha huduma ya maji.
Alisema vyombo hivyo vinahudumia maeneo makubwa ambayo ni kata zaidi ya moja hivyo wanafanya ni namna gani wanaboresha huduma za maji ili kuhakikisha tunafikia Ile asilimia85 ya upatikanaji wa huduma ya maji ifikapo mwezi juni kabla October.
Akizungumza kwa niaba washiriki Filbert Kalebo ambaye pia ni mhasibu wa chombo cha huduma ya maji korogwe amesema wanaishukuru serikali hivyo Watafanya kama watakapoelekezwa kwenye mafunzo.
0 Comments