Na John Walter -Babati
Katika kuadhimisha Ijumaa Kuu, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kupitia makanisa yake yote yaliyopo Wilaya ya Babati, iliungana kwa pamoja kufanya maombi maalum kwa ajili ya kuliombea taifa la Tanzania na viongozi wake wote.
Ibada hiyo takatifu ilifanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), usharika wa Babati Mjini, Jimbo la Babati, Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Maombi hayo yalilenga hasa kuliombea Taifa na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka huu wa Madiwani , wabunge na Rais uwe wa amani, haki na utulivu.
Aidha, viongozi wa dini waliomba kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na viongozi wote wa ngazi mbalimbali kuanzia vitongoji hadi taifa zima.
Katika maombi Wachungaji waliikemea vikali roho ya kutotenda haki na roho ya unyanyasaji, wakisisitiza umuhimu wa viongozi na wananchi kuzingatia maadili mema, haki na uwajibikaji katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Ibada hiyo iliudhuriwa na waumini zaidi ya 2,000 na kuongozwa na Mkuu wa Jimbo la Babati, Mchungaji Robert Mallya.
Katika ujumbe wake, Mchungaji Mallya aliwataka Watanzania kudumisha mshikamano, upendo na kumtanguliza Mungu katika kila hatua ya maisha yao.
Picha mbalimbali katika ibada hiyo
0 Comments