F Msaada wa kisheria wawafikia wakazi wa Tanga (Mama Samia leagal Aid) | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Msaada wa kisheria wawafikia wakazi wa Tanga (Mama Samia leagal Aid)


NA REBECA DUWE TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batlida Burian amewataka wananchi  wenye migogoro mbalimbali ikiwemo ya ndoa na ardhi  kujitokeza kwa  katika kampeni ya msaada wa kisheria  ya Mama Samia ambayo itafanyika kwa siku tisa katika kata zaidi ya 100  zilipo katika Halmshauri  zote 11 za mkoani hapa.

Kampeni hiyo, ambayo tayari imeshafanyika katika mikoa 22 ya Tanzania Bara, imeweza kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 2.2 na kushughulikia jumla ya migogoro elfu 20,000, ambapo migogoro zaidi ya 4000 imeweza kutatuliwa na kumalizika kabisa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini  kwake Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa kampeni hiyo si yalele  mama hivyo amewataka wananchi watoe taarifa za ukweli na za uhakika ili waweze kupatiwa msaada wa kisheria.

Kwa upande wake Laurent Burilo ambaye ni Afisa Uchunguzi Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria na Mratibu wa kampeni hiyo  alisema kuwa   changamoto zote  walizokutana nazo katika mikoa hiyo 22 ambayo tayari wamepita kuzitatua kisheria.

Alisema miongoni mwa Migogoro ya Ardhi, Mirathi na  ndoa ambayo  inahatarisha amani na usalama wa familia na jamii, na wakati mwingine husababisha mivutano isiyokwisha, ambayo inazuia maendeleo na ushirikiano.

Burilo aliongeza kusema kuwa  ni muhimu kwa jamii kuhamasika kutatua migogoro hii kwa njia ya amani ili kudumisha umoja na ushirikiano.

Post a Comment

0 Comments