Na Rebeca Duwe Tanga
MKuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani amewataka wananchi wa wa mkoa wa Tanga wenye Migogoro mbalimbali ikiwemo ndoa ,ukatili wa kijinsia vitendo vya ulawiti kwa watoto wa kike na wa kiume katika jamii ,wanawake na makundi maalumu na wale wenye migogoro ya ardhi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Kampeni ya msaada ya sheria ya Mama Samia itakayoanza rasmi kesho April 8
Hayo aliyasema wakati akifungua mafunzo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa mkoa Tanga ya wataalamu mbalimbali wakiwemo wanasheria wa kujitegemea,wanasheria wa serikali, polisi Dawati,na maafisa maendeleo kutoka halmashauri zote 11 ili kuweza kuwafikia wananchi wa mkoa huo katika siku tisa za kampeni hiyo ambapo itahitimishwa April 17 .
Aidha Batlida alieleza kuwa kamapeni hiyo katika mkoa wa Tanga itazinduliwa rasmi kesho tarehe 8 April katika viwanja wa vya Tangamano jijini Tanga ambapo tarehe 9 wataalamu watatawanyika kuendelea kutoa huduma hizo katika kata zote na vijiji na mitaa yote katika halmashauri zote za mkoa huo.
Samabamba na hayo alitoa wito kwa wataalam wote kuwafikia wananchi wote kama ambavyo wamekusudia kuwafikia na kuweza kusaidia wale wenye changamoto ya migororo ya muda mrefu.
Kwa upande wake MKurugenzi wa Huduma za msaada wa Sheria Esta Msambazi alisema kuwa lengo kampeni hiyo nikuweza kuwafikia wananchi kwenye ngazi ya vijiji wenye changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi ili kuweza kuwapunguzia idadi kuwaya watu wanaofikia katika ofisi ya mkoa ili watatuliwe migogoro yao.
Alisema kwamba kampeni imekuwa na mafanikio makubwa kwani wametatua migogoro ya aina mbalimbali na kuweza kuwafikia mtu mmoja mmoja zaidi ya milioni 2.2 katika mikoa 22 ambapo Jana wamekamilisha mkoa wa Arusha na kesho mkoa wa Tanga ambao ndio wa 24.
0 Comments