SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania Tasac, ambayo inayohusika na udhibiti wa huduma za usafiri majini imesema kuwa miongoni mwa changamoto kubwa iliyopo ni wadau wanaowahudumia kutokufuata utaratibu na sheria hususani wanapoomba leseni.
Hayo aliyasema mkurugenzi wa udhibiti wa usafiri kwa njia ya maji wa shirika la uwakala wa meli Tanzania TASAC Nelson Mlali wakati wa mafunzo ya elimu kwa watoa huduma ambao ni wale wanaowadhibiti ili wa wawe na uelewa mkubwa juu ya huduma hizo wanazotoa.
Alisema lengo kuu la kutoa elimu hiyo ni kuleta uelewa kwa wahusika ambao ni Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA, Wakala wa forodha na meli,wanaokusanya mizigo na kupunguza migogoro inayotokea baina ya watoa huduma.
"Wapo watu wasiowaamimifu ambao wanashindwa kufuata utaratibu na sheria hivyo kupitia elimu hii tunawapa uelewa wa madhara ambayo yatatokea wasipofuata utaratibu na kuweza kupata kupunguza changamoto hizo".alisema Mlali
Sambamba na hayo Mlali alitoa wito kwa watoa huduma kushirikina katika Majukumu kwa sababu wote katika jukuma la kufikisha huduma ili kuweza kupunguza malalamiko na migororo inayotokana na ukiukwaji wa sheria.
"Majukumu wa TASAC katika udhibiti wa huduma za usafiri wa majini ni kutoa ,kuhuisha na kufuta leseni za watoa huduma katika sekta ya bandani na usafiri kwa njia maji. lakini pia tumeweka kanuni na masharti ya kufuatwa na watoa huduma wanaodhibitiwa ."aliongeza MLali.
Mlali alisema kwa kutofuata Sheria na taratibu za utoaji wa huduma kwa wadau hao kutashusha kiwango cha ufanisi AA bandari zilizopo hapa nchini na kuifanya kuingia kwenye ushindani na nchi nyingine hali ambayo inaweza kupelekea wafanyabiashara kwenda kufanya kazi nje.
"Lengo letu kubwa ni kukaa nao tuone ni maeneo gani ambayo hayafanyi vizuri ili waweze kufanya vizuri kwaajili ya faida ya bandari zetu hapa nchini tungependa pia tupunguze malalamiko, migogoro na ucheleweshwaji wa utoaji huduma za usafiri kwa
Kwa upande wake Afisa mfawidhii kutoka shirika la uwakala wa' Meli Tanzania 'TASAC' mkoa wa Tanga Christopher Shalua amewataka wadau wa usafirishaji kwa njia ya maji kuhakikisha kupitia sekta zao za afya wanazingatia usalama kabla na baada ya kutoa huduma za kupakuwa na kupakia mizigo kweli Meli hususani zinazotoka nje ya nchi.
"Eneo la bandari ni eneo ambalo Lina mashara mengi kuna taasisi ambazo zinafanya kazi zao bila kujua kwamba wanaweza wakaingiza magonjwa hapa nchini Kuna baadhi ya takataka zianzokuja kwetu kwa njia ya Meli zinazotoka nje watu wa sekta ya afya lazima wahakikishe kwa nafasi zao hakuna madhara yanayotokea kwenye nchi yetu kupitia vyombo tunavyohudumia" alisisitiza Shalua.
Aidha afisa huyo amewataka wadau wote wa usafirishaji kwa jia ya maji kuhakikisha wanafuata Sheria na taratibu za nchi ikiwemo kuhusiaha lwseni zao ili waweze kupata ruhusa ya kufanya kazi zao bandarini wakati wote.
"Mawakala na wadau wote wanaotoa huduma za bandari lazima kuhakikisha kuwa vibali vyao vinahuishwa ili kufuata taratibu na Sheria za nchi yetu katika utoaji wa huduma bandarini" ameongeza
0 Comments