Mwenge waweka jiwe la msingi chuo cha VETA Kiteto.


Na John Walter -Kiteto 
Mwenge wa uhuru umeweka jiwe la msingi ujenzi wa chuo cha ufundi stadi (VETA) Wilaya ya Kiteto utakaogharimu Shilingi zaidi ya shilingi Bilioni 1 hadi kukamilika.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka huu Godfrey Mnzava ameridhishwa na hatua zinazoendelea katika ujenzi huo huku akiuagiza uongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa thamani halisi.

Taarifa ya mkuu wa wilaya iliyosomwa mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa, imeeleza kuwa ujenzi ulianza agosti 2023 na matarajio ya kukamilika ni agosti 2024 na mradi umefikia asilimia 25.

Aidha Mradi huo utakuwa na uwezo wa kuchukua Wanafunzi 353 kwa Pamoja hatua itakayosaidia kukuza ujuzi wa mafundi katika wilaya ya Kiteto na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira.

Kaulimbiu ya mbio za Mwenge wa uhuru 2024, Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Ujenzi wa taifa endelevu.

Post a Comment

0 Comments