Mufti Mkuu awataka Watanzania kupendeza na Kanzu hizi

Muft Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir amewataka watanzania na waislamu kwa ujumla kupendeza kwa kuvaa mavazi yanayotengenezwa na kampuni ya mzawa Mussa Bakari ya ‘Islamic Fashion Tanzania’.

Kiongozi huyo waislamu ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampuni hiyo ya mavazi ya kiislamu Tanzania na kueleza kuwa kwa mujibu wa maandiko ya dini hiyo, wameamrishwa kupendeza kwani Mungu wao ni mzuri na na hupenda vitu vizuri Alisema Muft Abubakar.
Muft Abubakar amefafanua kuwa uislamu huambatana na usafi na usafi huo unaanzia kwenye mavazi, hivyo ni vyema waislamu wakaitumia fursa hiyo kwa kununua mavazi kutoka kwenye kampuni hiyo ya mzawa.

Pia Muft ameshauri wazidi kujitangaza zaidi kwani huitaji wa vazi hilo ni mkubwa nchi nzima na sio tu kwa mkoa wa Dar es Salaam, huku akiwaomba wenye kampuni hiyo ikibidi watume muwakilishi kwenye sherehe za Eid El Fitr zinazotaraji kufanyika Mkoani Kilimanjaro kitaifa, ili wakazitangaze bidhaa zao na huko.

Muft Abubakar ameongeza kuwa ni vyema pia waislamu wakaambizana habari njema za ujio wa Islamic Fashion Tanzania ili wengi waweze kunufaika kwa kupendeza na mavazi yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Islamic Fashion Tanzania Mussa Bakari ameeleza kuwa kampuni hiyo imeanza tangu mwaka 2014 ambapo walikuwa wanategemea mavazi hayo kutoka nchi za nje, kutokana na jitihada walizofanya kwasasa wameweza kutengeneza mavazi yao ambapo nusu ya uzalishaji inafanyika Dubai na kumalizikia Tanzania.
Mkurugenzi Mussa Bakari ameongeza kuwa changamoto ya watanznia kukosa kanzu zenye ubora kwa muda mrefu ndiyo zimewapelekea wao kuanzisha Islamic Fashion Tanzania, ili kuwarahisishia watanzania waliokuwa wanasafiri kwenda nje ya nchi ili wapate kanzu zenye ubora.

Hivyo amewaomba watanzania kumuunga mkono ili aweze kupiga hatua zaidi za kuwahudumia watanzania.