Ng’ombe mmoja mjamzito kutoka nchi ya Bulgaria amehukumiwa kufa baada ya kuvuka mpaka wa nchi yake na kuelekea Serbia kinyume na sheria zinazongoza wanyama pori nchini humo.
Ng’ombe huyo ambaye amepewa jina la Penka alifanikiwa kuvunja zizi lake lililopo katika kijiji cha Kopilovtsi nchini Bulgaria karibu kabisa na mpaka wa Serbia na kuingia kimakosa katika mipaka ya nchi hiyo.
Mmiliki wa ng’ombe huyo Ivan Haralampiev pamoja na mtoto wake wamekuwa wakimtafuta ng’ombe huyo bila mafanikio mpaka walipopata taarifa kuwa anashikiliwa nchini Serbia.
Ikumbukwe kuwa nchi ya Serbia sio mwanachama wa Umoja wa Ulaya hivyo ili mnyama aweze kuruhusiwa kuingia katika nchi hiyo kutoka nchi wanachama Umoja wa Ulaya inabidi awe na vibali maalumu ili aruhusiwe tofauti na hapo sheria inasema kuwa adhabu yake ni kifo.