F Jifunze jinsi ya kupangilia sebule yako. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Jifunze jinsi ya kupangilia sebule yako.

Katika kipengele cha mitindo na utanashati, leo tutajikita katika kuangalia mpangilio wa veranda au sebule kama inavyofahamika na wengi.

Katika familia za kiafrika, sebule ni eneo muhimu ndani ya nyumba kwani ndiyo sehemu ya kwanza, ambayo mgeni hufikia kabla ya kujua maeneo mengine.

Ni eneo linaloweza kumjengea mtu au watu picha ya kujua wanaoishi ndani ya nyumba husika kutokana na mwonekano wa haraka haraka wa sehemu hiyo.

Endapo sebule itakosa mpangilio mzuri na unaoleweka, hata anayeishi ndani ya nyumba hiyo ataonekana hovyo.

Kutokana na hali hiyo ni vyema kuzingatia dondoo zifuatazo ili kuhakikisha sebule inakuwa na mwonekano mzuri kuliko eneo lolote ndani ya nyumba.

Mpangilio wa sebule kwa jumla
Ili kuhakikisha sebule ina mwonekano mzuri ni lazima kuwepo na mpangilio, utakaoonyesha kila kilichomo ndani ya eneo hilo kwa nafasi yake.

Siyo lazima yawepo makochi ya gharama sana ili nyumba iwe na mwonekano mzuri, yanaweza kuwapo hata makochi ya kawaida, lakini yakapangiliwa kwa mtindo unaofaa, yakapendezesha nyumba.

Epuka kurundika vitu visivyo na ulazima wa kukaa sebuleni kama vile viatu, nguo, chupa na vitu vingine vinavyoweza kuleta picha mbaya vikiwapo eneo hilo.

Sebule inapendeza zaidi ikiwa na vitu vichache, vitakavyowekwa katika mpangilio sahihi na kulifanya eneo hilo kuwa na mvuto wa aina yake.

Makochi, meza ya kawaida na meza au kabati la kuwekea runinga na redio, ndiyo vitu vinavyopaswa kuwapo sebuleni na siyo vinginevyo.


Mapambo
Watu wengi hususan wanawake, hupenda kurembesha sebule zao kwa mapambo mbalimbali, wakati mwingine bila kufahamu kuwa mapambo hayo yanaweza kuharibu mwonekano wa nyumba.

Sebule ya kisasa, haipaswi kuwa na mapambo mengi zaidi ya samani na rangi ya kuta. Kwa jumla, hivyo vinaweza kuifanya sebule iwe na mvuto wa hali ya juu.

Fremu chache za ukutani, ambazo zinaweza kuwa za maua au picha nazo zina uwezo wa kuleta nakshi ya aina yake katika sebule na kuifanya ivutie na kupendeza.

Usafi
Pamoja na kuwa unaweza kuweka samani za bei ghali, lakini suala la usafi linapaswa kuwa muhimu zaidi ndani ya nyumba kwa kuhakikisha muda wote sebule inapitika na kutazamika.