Zifutazo ndizo faida za kutumia pilipili hoho kiafya.
- Pilipili hoho huongeza kinga ya mwili. Hii husaidia mwili kupambana na magonjwa mbalimbali.
- Uwezo wa kupambana na magonjwa sugu ya saratani. Tafiti mbalimbali zimefanyika kuthibitisha hili.
- Husaidia kuongeza uwezo wa kuona kwa wale wenye matatizo ya macho. Hivyo ni vyema kutumia kiungo hiki cha chakula ili kuongeza uwezo wa kuona vizuri.
- Pilipili hoho husaidia mwili kupambana na magonjwa ya moyo.
- Juisi ya pilipili hoho husaidia kuchuja takamwili.
- Hutibu muwasho wa vidonda vya kooni.
- Pilipili hoho zina vitamini C kwa wingi hii husaidia kutibu ugonjwa wa kutokwa damu puani na kuimarisha kinga ya mwili.
- Husaidia kukinga saratani ya kibofu cha mkojo.
- Kupunguza mafuta yasio hitajika mwili hivyo huweza kupunguza uzito.
- Kuimarisha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kupunguza shinikizo la damu
- Huongeza kiwango cha damu mwilini.
- Husaidia mwili katika mfumo wa mmengenyo wa chakula.
- Mchanganyo wa juisi ya pilpili hoho na spinachi humaliza tatizo la kujaa kwa gesi tumboni.